Mrejesho, kumsahau mwenza

MUGUNDA

Member
Aug 11, 2011
69
62
Baada ya mwezi kupita mimi na wife tukiwa tumetengana nilipigiwa simu na Afande flan mwenye cheo cha Inspector na kuniomba nifike Kesho yake saa nne hasubui, bila kuchelewa nilifika kumbe wife alikuwa amenishitaki katika dawati la jinsia. Walitusuluhisha then wakaomba nimrudishe wife nyumban, nam nilikubaliana nao na sasa kurudi. Ila sasa ni wiki sasa katu hatuongei pamoja, tuko kitanda kimoja hatuongei, hanifungulii mlango nikirud anaegeshea tu, pili chakula nakikuta chumban kwenye hotpot lkn sikigus kutokana na kushituka, najiuliza baada ya kuja akiwa mpole yeye ndo kaongeza kabisa ukali wa kukaa kimya, nam nimeamua kukaa kimya tuone mshindi ni nan.
 
Endelea kukaa kimya tuone mahindi nani Ila usisahau kuleta mrejesho wa mshindi
 
Hhaahhahhaa... Ndoa hizi uwiii... Hahahaa.. Kazi kweli kweli...So for how long you both will keep doing that?? Hhahaaa.. I'm sorry but its very funny .. Wote mko juu eeeheee... Okay... Thanks..
Advice him nn cha kufanya.... M sure u went thru this situation....
 
We kweli huna maamuzi magumu ndomana anakuona pimbi tu..uanaume si kuwa na pumbu tu onyesha kwanini wewe ni mwanaume na siyo wa kiume..sa we endelea kusikiliza dawati la jinsia wakupelekepeleke kama gari bovu..
 
Baada ya mwezi kupita mimi na wife tukiwa tumetengana nilipigiwa simu na Afande flan mwenye cheo cha Inspector na kuniomba nifike Kesho yake saa nne hasubui, bila kuchelewa nilifika kumbe wife alikuwa amenishitaki katika dawati la jinsia. Walitusuluhisha then wakaomba nimrudishe wife nyumban, nam nilikubaliana nao na sasa kurudi. Ila sasa ni wiki sasa katu hatuongei pamoja, tuko kitanda kimoja hatuongei, hanifungulii mlango nikirud anaegeshea tu, pili chakula nakikuta chumban kwenye hotpot lkn sikigus kutokana na kushituka, najiuliza baada ya kuja akiwa mpole yeye ndo kaongeza kabisa ukali wa kukaa kimya, nam nimeamua kukaa kimya tuone mshindi ni nan.
sasa kwanini ulimrudisha nyumbani kama mlikuwa bado hamjawa tayari, ndio nyie mnaokufa kwa kukatwa NYETI wanawake hawasomeki, japo sijajua chanzo cha ugomvi, huwezi kuishi na mtu ndani ya nyumba kwa hali hiyo sio mwanao huyo. halafu unakuja hapa kujisifu nani mshindi, subiri siku ukiamka na kukuta nyeti ziko juu ya dressing table ndo utajua.
 
Ndugu soma ujumbe huu hapa chini utakusaidia

Alichosema mama kwa Kijana wake wa kiume siku moja kabla ya kufunga ndoa.

Mummy’s man!

Wewe sasa ni mwanaume. Kuanzia kesho utakuwa na mwanamke mwigine wa maisha yako. Mpishi mwingine na mtu mwingine wa kushare nae siri zako, sitakuwa mimi tena.

Mpende mwanamke wako pengine kuliko hata mimi. Kabla hujaenda jumla kuanza maisha mengine mwanangu acha nikupe maneno machache yatakayokuongoza;

Kuna siku nilikuwa sina maelewano mazuri na baba yako. Nilikuwa nikipiga kelele na kufoka hasira zilikuwa juu, nae hasira zake zilikua juu vilevile. Nikamtusi kwa kumwambia yeye ni "mpumbavu".

Alinishangaa!! Akaniuliza nathubutuje kumuita yeye mpumbavu? Hapo hapo nikamuongezea matusi mengine nikimuita mjinga, na hana busara, nilimuita majina yote mabaya.

Angalia unajua ni nini alifanya? Hakunyanyua mkono wake kunipiga. Aliondoka kimya kimya. Akabamiza mlango na kutokomea.

Mwanangu, kama baba yako angenipiga labda na kuniumiza, kunivunja either mkono au mguu, ungekaa na mimi hapa? Ungemuheshimu kama baba yako? Je ungekuwa unajivunia kuwa na baba kama yeye? Au ungenilaumu mimi kwa kumuita yale majina ya kuudhi.

Kamwe usimpige mkeo! Haijalishi amekuudhi kwa kiasi gani. Wewe kaa kimya na ondoka na mambo yatasonga. Kila atakapojaribu kuleta maudhi kumbuka haya niliyokueleza.

Kabla sijasahau, Baada ya baba yako kuondoka, nilijisikia vibaya mno. Alirudi akiwa bado na hasira. Na asubuhi siku iliyofuata nilifanya kila naloweza kumuomba msamaha.

Alinisamehe kwa moyo mweupe na siku hiyo nilimpikia chakula kizuri akipendacho, Yes najua unafahamu kuwa baba yako anapenda sana mboga za maboga zilizochanganywa na viazi mbatata.

Baada ya siku hiyo sikumuita tena majina ya kuudhi wala kumkasirisha. Heshima yangu kwake ilizidi maradufu.

Kuna kitu kikubwa cha muhimu ambacho unahitajika kukifanya kila siku, mwanangu nisikilize, mtetee mke wako.

Pale atakapokuwa under pressure simama nae kidete. Kama marafiki zako watamchukia ni jukumu lako kumfanya ajione kama ni malkia wa nguvu.

Baba zako wakubwa na wadogo hawakuwahi kunipenda, lakini baba yako siku zote alisimama upande wangu mpaka pale walipokuja kubadilika na kuniomba msamaha.

Kuna siku baba yako alikuwa mwenyeji wa mmiliki wa kampuni pamoja na wafanyakazi wenzake wawili alikokua akifanyia kazi, wote waliomba kujihifadhi hapa nyumbani kwetu.

Siku hiyo nilikuwa jikoni nikiwapikia chakula na baba yako alienda kununua vinywaji kwa ajili ya wageni. Baada ya kumaliza na kuandaa chakula mezani, kila mmoja alianza kula.

Ndipo nikakumbuka kuwa nilisahau kuweka chumvi katika chakula. Niliaibika mno mbele ya wageni. Baba yako baada ya kula tu kijiko cha kwanza alinitizama. Halafu hapohapo akawatazama wageni.

Akawaambia wageni kwamba alinipa maelekezo mwezi uliopita kwamba nisiwe naweka chumvi katika chakula kwa vile ana matatizo ya kiafya. Alizungumza hayo kwa utani mwingi na bashasha kuizima ile aibu.

Wageni walielewa na akaniomba niende nikachukue chumvi kila mmoja ajiwekee kivyake. Yeye alikula vilevile bila chumvi mpaka akamaliza. Baada ya wageni kuondoka alinihimiza tu kwa upole kuwa makini siku nyingine.

Mke wako ni kama mtoto, muda mwingine anaweza akashindwa cha kuongea au cha kufanya. Simama na ongea kwa ajili yake!

Tengeneza mazoea ya kwenda maeneo mbalimbali na mkeo, hiyo inampa ujasiri na kujiamini. Mbali na kazini, tembelea maeneo mengine na yeye.

Kama kuna mtu atakualika nyumbani kwake, au katika event yoyote ile na akakwambia usiende na mkeo kuwa makini na utumie busara.

Najua unanipenda mimi mama yako, najua huwa unanieleza matatizo na changamoto zako. Lakini kwa sasa mambo ni tofauti.

Mkeo awe wa kwanza kujua hayo kabla hujanieleza mkmi. Mwache yeye aone kabla yangu.

Kama unamatatizo nae usikimbilie kwangu. Acha siku ipite na uongee nae mwenyewe, na uombe Mungu kwa ajili ya hilo jambo.

Usishirikishe marafiki zako matatizo ya mkeo, kwao itakuwa burudani na watakucheka kinafiki kwa kushindwa kusimamia ustawi wa ndoa yako.

La mwisho, usisahau kuja kunitembelea wewe na mkeo kila mwezi. Najua utakuwa na nyumba yenye furaha, ila siku zote wewe bado ni mummy's Man.

Mungu atabariki nyumba yako na uzao wako. Usisahau kumuomba yeye na kutafuta msaada kwake.

Nimekulea katika maadili mema, Nimekusomesha, una elimu kubwa, basi ukawe mfano bora kwa kila kijana ulimwenguni, ukawatie moyo na kuwapa matumaini juu ya Ndoa.

Msingi wa taifa lolote lenye maadili huanzia katika ngazi ya familia. Hii ambayo wewe unaenda kuijenga.

Nitakupenda siku zote mwanangu, nenda na ninakutakia kila la kheri mwenyezi Mungu akubariki wewe, mkeo mtarajiwa na uzao wako.
 
Unanikumbusha mchapo wa wanandoa waliochuniana japo waliendelea kulala kitanda kimoja (mzungu wa nne). Wanawasiliana kwa maandishi kwenye karatasi, ambapo karatasi hiyo inawekwa mezani ili mwenzake aisome.

Siku moja mume akawa anasafari ya nje ya nchi kwa ndege. Akamwomba mkewe (kwa kikaratasi) kuwa amuamshe mapema alfajiri ili aiwahi ndege.

Mke alfajiri aliamka, akaandika ujumbe kwenye kikaratasi "Mume wangu amka kumekucha". Akiweka kikaratasi pale mezani na kurudi kulala kitandani.

Mume akazinduka usingizi, akacheki muda na kuona amesaliwa na dk 10 tu na airport ni mbali. Akaanza kumfokea mkewe kuwa kwa nini hakumwamsha.....

KEEP ON FIGHTING DUDE!!!
 
sasa kwanini ulimrudisha nyumbani kama mlikuwa bado hamjawa tayari, ndio nyie mnaokufa kwa kukatwa NYETI wanawake hawasomeki, japo sijajua chanzo cha ugomvi, huwezi kuishi na mtu ndani ya nyumba kwa hali hiyo sio mwanao huyo. halafu unakuja hapa kujisifu nani mshindi, subiri siku ukiamka na kukuta nyeti ziko juu ya dressing table ndo utajua.
Hahaaaaaaahhhaaa... Dear unammtisha mwenzio hhaaahaa yaani this is so much fun... Hahaa.. Thanks..
 
Ndiyo tatizo ya kusaidiwa kuwaza ndani ya maisha yako...So umekubali kurudiana kisa tu ulipigiwa simu na afande mwenye cheo cha Inspector...Maisha ni yako na ni wewe unaamua uishi kama upo paradiso ama kama upo jehanum...Na huwa nasema mwanaume ni kosa kubwa kununanuna kwa hiyo na wewe hadi mdomo unavuta...Ita mama bila kujali kanuna ama kavimba mweleze haya si maisha tunayoishi na nataka kwa usiku huu nieleze ni wapi nilipokukwaza na wewe umweleze kipi hupendi na unachopenda kutoka kwake...Then unganisheni mwili uwe mmoja usiku huo kesho yake na maji bafuni utawekewa karafuu..
 
Baada ya mwezi kupita mimi na wife tukiwa tumetengana nilipigiwa simu na Afande flan mwenye cheo cha Inspector na kuniomba nifike Kesho yake saa nne hasubui, bila kuchelewa nilifika kumbe wife alikuwa amenishitaki katika dawati la jinsia. Walitusuluhisha then wakaomba nimrudishe wife nyumban, nam nilikubaliana nao na sasa kurudi. Ila sasa ni wiki sasa katu hatuongei pamoja, tuko kitanda kimoja hatuongei, hanifungulii mlango nikirud anaegeshea tu, pili chakula nakikuta chumban kwenye hotpot lkn sikigus kutokana na kushituka, najiuliza baada ya kuja akiwa mpole yeye ndo kaongeza kabisa ukali wa kukaa kimya, nam nimeamua kukaa kimya tuone mshindi ni nan.

kaka naomba nikuulize swali moja tuu kabla sijakushauri; mna umri gani ndani ya ndoa? na je ndoa yenu mliifungia kanisani/msikitini au kwa DC? naomba unijibu harafu ntakushauri jambo kaka
 
Baada ya mwezi kupita mimi na wife tukiwa tumetengana nilipigiwa simu na Afande flan mwenye cheo cha Inspector na kuniomba nifike Kesho yake saa nne hasubui, bila kuchelewa nilifika kumbe wife alikuwa amenishitaki katika dawati la jinsia. Walitusuluhisha then wakaomba nimrudishe wife nyumban, nam nilikubaliana nao na sasa kurudi. Ila sasa ni wiki sasa katu hatuongei pamoja, tuko kitanda kimoja hatuongei, hanifungulii mlango nikirud anaegeshea tu, pili chakula nakikuta chumban kwenye hotpot lkn sikigus kutokana na kushituka, najiuliza baada ya kuja akiwa mpole yeye ndo kaongeza kabisa ukali wa kukaa kimya, nam nimeamua kukaa kimya tuone mshindi ni nan.
Mama mkwe wangu aliniambia jumapili kwamba ndoa ikivunjika au ikikosa maelewano mimi mwanaume ndie wakulaumiwa. Sababu ni kwamba mwanaume ndio kichwa cha nyumba na pia biblia inasema wanawake ni viumbe dhaifu na biblia inatutaka tuishi nao kwa akili. Take it
 
tumia akili yakiume, acha kununa kama mkeo mwanamke anatakiwa kubembelezwa nakuthaminiwa. Kuwa mpole na usululishe hilo swala lenu ili muwe sawa hata ukiendelea kuna haitasaidia kitu tumia nafasi yako kama kicha cha familia kuweka sawa hayo mambo yenu na usithubutu tena kuyatoa nje.
 
Endeleeni hivyo hivyo tu kadri mda unavyozidi kwenda mbele ntaanza kuongea,kusalimiana na mambo yatarudi kawaida hizo ni changamoto za ndoa.
 
Back
Top Bottom