Mramba alibebesha mzigo Baraza la Mawazir | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mramba alibebesha mzigo Baraza la Mawazir

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PROFESA KYANDO, Aug 24, 2012.

 1. PROFESA KYANDO

  PROFESA KYANDO Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=2][/h] Ijumaa, Agosti 24, 2012 05:48 Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

  ALIYEKUWA Waziri wa Fedha, Basil Mramba, ameiambia mahakama kuwa mkataba kati ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Kampuni ya Alex Stewart, ulisainiwa bila kujadiliwa na Baraza la Mawaziri wala Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuridhia.

  Mramba, alidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mjini Dar es Salaam, alipokuwa akijitetea mbele ya jopo la mahakimu, Sam Lumanyika, John Utamwa na Saul Kinemela, kwa kuongozwa na wakili wake, Hurbert Nyange.

  “Niliandika dokezo kwenda kwa Katibu Mkuu mmoja wa Wizara ya Fedha na kumweleza, kwamba sikudhani kama Gavana wa BoT angetiliana saini na Alex Stewart, bila kukubaliana na kujadiliana na Baraza la Mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuridhia.

  “Niliomba anipe ushauri kuhusu madai ya msamaha wa kodi yanayojitokeza katika mkataba, yanayotakiwa kuidhinishwa,” alidai Mramba.

  Alidai aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati huo, Daniel Yona, alimwarifu Rais Benjamin Mkapa majadiliano kati ya Mramba, Yona na Mwanasheria Mkuu wa Serikali yaliendelea vizuri, hivyo aliomba kibali cha kuruhusu Waziri wa Fedha na BoT, watafute fedha za kuilipa kampuni hiyo ili kazi ianze kufanyika.

  “Katibu Mkuu wa Rais, Patrick Mombo, alimwandikia Waziri wa Nishati na Madini barua Mei 13, 2003, akimweleza kuhusu huyo mkaguzi, Rais Mkapa akakubali, Wizara ya Fedha na BoT kutafuta fedha za kulipa ili kazi ianze,” alidai Mramba.

  Mshitakiwa huyo, alidai Rais Mkapa alihimiza wasaidizi wake waliohusika katika mkataba huo kutekeleza makubaliano haraka.

  Alidai Gavana Benki Kuu ya Tanzania, kwa mamlaka yake anaruhusiwa kuingia mikataba na kutoa msamaha wa kodi, hivyo katika mkataba kifungu cha 4.3.1, kinaeleza malipo yoyote yaliyokuwepo katika mkataba hayatatozwa kodi.

  “Mimi sikuruhusu msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart, nilichofanya ni kutekeleza matakwa ya mkataba ulioingiwa kati ya kampuni na BoT ya kusamehe kodi.

  “Tuliamua na kushauriwa kusamehe kodi ili kuachana na usumbufu mkubwa, kwani walitaka kupata asilimia 1.9 bila kupungua… tungekataa kodi Serikali ingetakiwa kutumia fedha nyingi zaidi,” alidai.

  Mramba, alidai baada ya kusainiwa mkataba huo, alimruhusu Gavana wa Benki Kuu (BoT) wakati huo, marehemu Daudi Balali, kuilipa Kampuni ya Alex Stewart, Dola za Marekani milioni moja kama malipo ya awali kwa ajili ya kazi hiyo na kuahidi Serikali ingezirejesha.

  Wakati kesi hiyo ikiendelea, Wakili Nyange alikumbana na vikwazo mbalimbali kutoka kwa mawakili wa Serikali na jopo la mahakimu, kutokana na kutumia nyaraka za Yona kumuuliza maswali Mramba, kurudia maswali ya juzi, kumwongoza majibu ya swali mteja wake na kujichanganya wakati wa kuuliza maswali hayo.

  Washitakiwa katika kesi hiyo, wanakabiliwa na mashitaka ya kutumia madaraka vibaya na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 11.9 kutokana na uamuzi wa kuipatia msamaha wa kodi, Kampuni ya Alex Stewart. Kesi hiyo, itaendelea Oktoba 12, mwaka huu.
   
 2. a

  afwe JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Hii nayo ni movie nyingine ya serikali! Mwisho wa siku Mkapa atajitosa na kusema alitoa baraka zote kama ilivyoelezwa kama rais wa nchi. Ngoja tuone!
   
Loading...