Mradi wa upimaji viwanja-Mkuranga

Mradi wa upimaji viwanja-Mkuranga

Simburya

Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
30
Reaction score
8
Heshima mbele wana JF,

Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa maada katika jukwaa hili,Kwa sasa nimeona vyema kurudi jamvini kueleza maendeleo ya project yangu na inaweza kusaidi kupata msaada mkubwa wa mchango kwani naamini hapa ni kitovu cha taaluma na ujuzi wa mambo na pia watu wanaweza kujifunza jambo fulani kupitia wazo langu hili.

Kuna watu wamekuwa wakinitia hamasa kila nikisoma maada zao wanazozianzisha. Kwa muda mrefu nimekuwa nikiwaza kuanzisha kitu ambacho kitaniingizia fedha kubwa!! Muda mwingi tunagombea fursa za kuajiriwa bila kutambua kuwa kuna fursa nyingi tu ambazo tumezilalia ama tunabweteka na ajira tulizonazo bila kutafuta chanzo mbadala cha mapato.


Kwa sasa nimeajiriwa lakini nina mawazo mengi ya kijasiriamali na panapo majaaliwa kama huu mradi utafanikiwa basi nitatimiza ndoto zangu za kuwa na kitu changu ninachoweza kukisimamia mwenyewe.


Nikiwa kazini Mkoa wa Pwani niliona fursa adhimu kwenye "maeneo" na nilijitahidi kununua vieneo vichache kwa kadri fursa ya kipato ilivyoruhusu.


Baada ya muda kupita nikaja kugundua kuwa maeneo mengi yanayouzwa na Halmashauri za mkoa tajwa ni ya wazawa ila kuna makubaliano yameingiwa kati ya wenye maeneo a Halmashauri ili kuendeleza maeneo husika na kuyapima.Hivyo nikajisemea moyoni kuwa hata mimi nikiwa na eneo langu basi nitaweza kulipima na kuuza viwanja.


Baada ya muda nilipata mdau mwingine mwenye maono sawa na yangu tukaamua kutafuta eneo Kibaha (hekari 50) na kufanikiwa kupata mchoro wa Mipango miji ambao ulipitia vikao vya halmashauri, Ofisi ya mipango miji/Ardhi mkoa na Wizarani. Ikawa imebaki phase II ya mradi ya ?surveyor? kuanza kazi ya kupanda mawe(beacons) na kuandaa surveyed plan.. Hakuna safari isiyo na mabonde, wakati tukiwa tumeanza hilo zoezi wakajitokeza watu wakisema eneo tajwa ni mali yao na kesi ikaanza kuunguruma..(Hadi sasa kesi imetoka kituoni imehamia mahakamani ila Mungu mwema ataingilia kwenye hili maana hakuna haki ya mtu itakayozikwa)


Sababu mambo ya kesi huchukua muda tukajikusanya tena na kuamua kuanza tena project katika eneo linguine huku wakati huu tukijipanga vyema zaidi ili lisitokee lililotokea Kibaha.. Tukaamua kwenda Mkuranga ambapo tulibahatika kupata heka 63 mwezi wa nane(8) mwishoni... Tukafuata taratibu tena za kuandaa mchoro wa mipango miji na kupitisha kwenye vikao vya Halmashauri, ofisi ya Ardhi mkoani na Wizarani. Mungu amesaidia sasa ramani imeshakuwa approved Wizarani na surveyor yupo site ameanza kazi.



Hii ni project inayolipa sana na nitawapa mchanganuo kwa ufupi kwa kutumia makadirio ya hekari 50.


  • Eneo Mkuranga heka 50@1.5Mil...................................75Mil
  • 10% ya kijiji kama atalipa mnunuzi wa eneo???????? 7.5Mil
  • Town planner wa kuandaa mchoro(mipango miji)????.. 6Mil
  • Surveyor wa kuweka beacons na kuandaa mchoro?????15Mil
  • Miscleneous.............................................................. 3Mil
Jumla ni ?????????????????????????????.....106.5Mil

Bei itategema na ushawishi wa kuomba punguzo(discount) maana maeneo yanaanzia 1Mil hadi 1.5 Mil ambayo hayapo ndanindani sana..

Pia kwa Town planner na Surveyor pia itategemea na mazungumzo kati yenu.

10% ni makubaliano ya mnunuaji na muuzaji.. kama utachangia 5% nay eye 5% , am azote zitalipwa nawe ana nay eye kutegemea na situation

Upande wa mapato-Roughly

Ukiwa na heka 50 roughly unaweza baki na heka 38 (heka 12 zikatumika kwenye open space na barabara za mitaa kwenye eneo husika)

Heka 38 ni sawa na mita za mraba 155,496 (tumekadiria heka 1 ni sawa na mita za mraba 4092)

Hivyo utakuwa umeweka sokoni viwanja vyenye jumla ya mita za mraba 155,496
Bei ya sokoni ya mita moja ya mraba kwasasa ni Shs 5000/=

Shs 5000*15,496 ni sawa na Tsh 636,289,632
Inachukua miezi si chini ya minne kukamilisha hii project? Inalipa kutumia 100Mil kutengeneza 600Mil.

Nimejifunza kuwa uvumilivu unalipa sana na unapokata tama ndipo mafanikio yanapokuwa yamekaribia.

Changamoto


  • Ofisi zetu za Serikali zina urasimu sana hivyo document inachukua muda mrefu sana kupita ofisi moja kwenda ofisi nyingine,
  • Njia madhubuti ya kuuza viwanja ili pesa ipatikane kwa wakati.
  • Kupata mtaji wa kujiingiza kwenye hii biashara
Kwa hii project inayoendelea sasa tumepata viwanja visivyopungua 240 ambavyo ifikapo trh 20January panapo majaaliwa vitakuwa sokoni.Kati ya hivyo kuna vya makazi/makazi na biashara/na nursery. Bado tunatafakari njia bora ya kuviuza maana ya kushirikiana na halmashauri nayo ina process ndefu sana tukitumia uzoefu tuliopitia mwanzo.


Haya wadau naomba mawazo yenu kwenye hili tujijenge na kuona nini cha kufanya. Ninasikiliza mawazo yenu na ushauri! unaweza kuchangia au kuniPM vyovyote utakavyoona

Ahsanteni sana
 
Ongea na makampuni binafsi,pamoja na serikali uwakopeshe waalim kwa mkopo wa mwaka 1.
 
Hello Rene
Kwa sasa hatuna kampuni sisi ni watu binafsi.Tuna ndoto za kufungua kampuni ili tuwe formal zaidi.
Asante


QUOTE=Rene Jr.;14760505]Safi sana, kampuni yenu inaitwaje?[/QUOTE]
 
Aisee bonge la wazo mkuu.
Ila nakushauri saana wakati wa kununua tumia mwanasheria.
Maana mwanzo mlipigwa,sasa sijui wapi mlieteleza.Maana hawa watu wa halamshauri nao ni wapiga dili sana.Ila serikali hii wataumbuka.

Ni kweli maeneo ya mkuranga viwanja kwa bei ya 5,000 kwa mita za mraba ndio bei yake,niliwahi kuja huko.Kununua cha serikali.Ila mbali aisee,panda shuka duuhh.Nimekiweka huko mtu analima matembele na mihogo.
Ila ni mjia unaokuwa kwa mipango ya kisasa sana,maana makampuni makubwa yamekata viwanja huko.

Mie najiuliza hivi:
Imekuwaje umeweza kuwekeza kwenye biashara kubwa kama hiyo bila haya kuwa na kampuni uchwara?
Maana kama ukiuza hata kiwanja kimoja kwa mfumo wako huo ni bonge la kesi,unless utafute ubia na Halmashauri wauze wao na mpange nani atalipia VAT.
 
Je mleta uzi hongera sana. Mimi nina Heka 10 Malogoro Mkuranga. Ninataka nifanye utaratibu kama huu.
 
Je mleta uzi hongera sana. Mimi nina Heka 10 Malogoro Mkuranga. Ninataka nifanye utaratibu kama huu.
Nadhani hukumuelewa waziri Lukuvi.

Ameshasema hiyo biashara hakuna tena.

Mwisho akasema waliokuwa na mashamba halafu wanataka kupima viwanja "imekula kwao".

Nakushauri kalisajiri kama shamba, lipande miti ya mitiki. Ili watoto wako waje kufaidi baada ya miaka 25 ijayo.
 
Nadhani hukumuelewa waziri Lukuvi.

Ameshasema hiyo biashara hakuna tena.

Mwisho akasema waliokuwa na mashamba halafu wanataka kupima viwanja "imekula kwao".

Nakushauri kalisajiri kama shamba, lipande miti ya mitiki. Ili watoto wako waje kufaidi baada ya miaka 25 ijayo.
Aksante sana nakushukuru kwa maono.
 
Je mleta uzi hongera sana. Mimi nina Heka 10 Malogoro Mkuranga. Ninataka nifanye utaratibu kama huu.
Asante mkuu.
Kwasasa haitakuwa rahisi tena kupima eneo kwa mtu binafsi kama tulivyofanya sisi hadi Mh. Waziri atakaposema vinginevyo.

Sisi pia tulutamani kufanya project kama hizi nyingi ila haitawezekana kwasasa.

Kama nilivyoleta uzi huu kuwa taratibu za kupima zikichukua mzunguko mrefu kuanzia halmashauri kwenye vikao vya mipango miji hadi wizarani.. Na Mungu mwema kazi yetu imetoka Wizarani.

Kama utaratibu wa zamani ukirejeshwa usisite kurejelea uzi huu maana nikielezea mtiririko wa hatua za kufanya.
Asante
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom