Mradi wa maji uliokwama kwa miaka 11 wakamilishwa na Serikali ya Rais Samia

Mradi wa maji uliokwama kwa miaka 11 wakamilishwa na Serikali ya Rais Samia

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mradi wa Maji wa Same–Mwanga–Korogwe ulianza rasmi mwaka 2014 baada ya utafiti wa awali kuanza mwaka 2006, lakini ulikwama kwa takriban miaka 20 kutokana na changamoto za kifedha, usimamizi, na mabadiliko ya mikataba.

Soma pia: Rais Samia azindua Mradi wa Maji Same-Mwanga-Korogwe Machi 9, 2025

Screenshot 2025-09-09 011546.png

Serikali ya Rais Samia ilianza juhudi za kuufufua mradi huu, na hatimaye ulizinduliwa rasmi tarehe 9 Machi 2025, baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza.

Awamu hii ilikamilika mwaka 2024 ikiwa na uwezo wa kutoa lita milioni 51.6 za maji kwa siku na inawanufaisha zaidi ya wananchi 456,000 katika wilaya za Same, Mwanga, na Korogwe.

Kwa ujumla, mradi huu umechukua takriban miaka 11 tangu kuanza kwa ujenzi hadi uzinduzi rasmi, na takribani miaka 20 tangu utafiti wa awali, jambo linalothibitisha juhudi kubwa za Serikali ya Rais Samia katika kukamilisha miradi iliyokwama na kuhakikisha upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi.
 
Hiyo miaka 11 Chadema ndiyo walikuwa madarakani mpaka mradi ukwame?
Hii nchi ili uelewe CCM unatakiwa uwe mjinga Kuna wajinga watapiga makofi hapo kumpongeza
 
Unawataarifu watu wa nchi gani? Mbona mnakosa akili na aibu kiasi hiki?
 
Mmeipiga pini jamiiforum na mnaleta habari zenu huku?
Moderator
Mtandao wa X, serikali wameifungia na bila VPN hutoboi ila utakuta habari za serikali wanapost huko baada ya muda.
Utashangaa Mama Abdul naye yupo Jamii forum muda huu anaperuzi
 
Hao uaowanadi wamefungia huu mtandao still bado mnakuja kuwapamba huku
 
Kuna jamaa yangu mmoja mitaa hiyo ya Bahi aliwahi kuwa ananitania kwamba ule mradi ulikwamishwa na serikali ya nchi ile ya upande ule wa mashariki (rejea riwaya ya kusadikika) ya F. Topan na kwamba serikali ya CCM ndo itakuja kuukomboa huo mradi.

Nilikaa miaka mingi sana pasipo kuelewa maana ya ile sentensi hadi leo hii ndo naelewa kumbe ile ilikuwa ni riwaya ya "nchi inayoitwa ya kusadikika" na kimsingi kumbe ile nchi haijawahi kuwepo kokote ulimwenguni japo ilionekana katika matendo yake kuwa mengi. Sasa kama ile nchi ilikuwa ni ya kusadikika tu na haijawahi kuwepo yafaa sasa, serikali hii ya CCM ambayo inasema imeukomboa huo mradi basi waseme ni serikali ya nchi gani ilikwenda kuukwamisha huo mradi Ili tuamini kweli ulikwamishwa na X na sasa umekombolewa na Y
 
Back
Top Bottom