Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,802
- 34,193
Afisa Mahusiano wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud
MRADI mkubwa wa umeme wa gesi kupitia bomba kubwa kutoka Mtwara na Lindi hadi Kinyerezi jijini Dar es Salaam umekamilika na kwamba wananchi wameanza kunufaika. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).
Uthibitisho huo, umetolewa leo na msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema kuwa mradi huo ulianzishwa ili kusaidia Watanzania kuondokana na shida ya umeme na kwamba utawezesha Taifa kupata umeme wa uhakika na gharama nafuu.
“Mradi huu utasaidia kuokoa sh.1.6 trilioni, zinazotumika kununulia mafuta ya kuzalishia umeme,” amesema.
Kwa mujibu wa Badra, umeme wa gesi una faida kubwa kwa wananchi wa hali ya chini kwa vile unapatikana kwa bei nafuu na hautegemei maji wala mabadiliko ya hali ya hewa kama umeme wa kawaida.
Badra emefafanua kuwa, mradi huu umekuwa chachu ya maendeleo ya viwanda nchini kwani vingi vimeonesha nia ya kutumia nishati ya gesi asilia katika kuendesha mitambo yake ya uzalishaji.
“Kukamilika kwa mradi huu pia kutachochea matumizi ya gesi asilia majumbani, na katika shughuri za usafilishaji, hivyo kupunguza uchafuzi wa mazingira, matumizi ya mkaa na kuni nchini.
“Tatizo la ajira pia litapungua kutokana na kuongezeka kwa viwanda na biashara,” amesema Badra.
Ameongeza kuwa, mradi utawanufaisha zaidi wananchi ambao wanakaa katika maeneo yote ambayo nguzo za umeme zitapita na mabomba ya gesi. Kwamba watalipa sh. 2,7000 na watapatiwa huduma za maji bure.
“Tumefanya hivyo ili kuwahamasisha wakazi wa maeneo hayo watambue umuhimu wa gesi na jinsi ya kutunza mazingira. Pia tunatoa elimu bure juu ya matumizi ya gesi asilia na faida zake, hivyo tunawafanya wawe walinzi wazuri wa mazingira na mabomba ya gesi yaliyopita kwenye maeneo yao,” amesema.
Hata hivyo, Badra amesema, Serikali kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini wanatoa fursa kwa Watanzania 10 kwa kuwapatia nafasi za masomo chini ya ufadhili wa Serikali ya China, katika ngazi ya shahada ya juu ya uzamili katika fani ya gesi na mafuta katika Chuo kikuu cha China.
Waombaji wa nafasi hizo wanatakiwa kuwa na shahada ya Sayansi ya Ardhi au Uhandisi kutoka vyuo vinavyotambulika na serikali, mwenye umri wa miaka kati ya 35 hadi 40.
chanzo.Mradi wa gesi kutoka Mtwara wakamilika