‘Mr Nice’ ameibuka upyaaa!

RAKI BIG

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
394
456
MSANII aliyejizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya Bongo miaka ya 2000, Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ ameibuka upyaaa!

Safari hii fujo na makeke yake yanatokea nchini Kenya ambako ameweka makazi yake baada ya kukimbia ukata wa Bongo.

Maisha ya mshikaji yamebadilika kwa kiasi kikubwa; Mr Nice wa Kenya siyo yule aliyekuwa analala baa hapa Tanzania.

Mabadiliko hayo ya kimaisha yamewaacha watu wanashangaa na kujiuliza, jamaa ametoboaje kwenye maisha magumu?

Msanii huyo alizungumza hivi karibuni na Amani kwa njia ya mtandao wa WhatsAap na kusema kuwa, ameamua kuhamishia shughuli zake za muziki nchini Kenya, kwa sababu watu wa huko wanakubali kazi zake.

Alisema, Wabongo wamesahau makali yake kwa sababu ya kile alichodai wanapenda kusikiliza nyimbo za matusi.

“Nahisi ningebaki Bongo, ningeweza kufa kwa stress maana mtu anajifanya amesahau hata nyimbo zako wakati nchi ya jirani wanazipenda na hata kukupa shoo.

“Wabongo wengi kazi yao kubwa ni uzushi tu na si kitu kingine chochote,” anasema Mr Nice.

Mr Nice anasema kwa sasa amepata mafanikio makubwa kiasi cha kuweza kuanzisha mradi wake wa maji ya kunywa ambayo yanaitwa Nice Water.

“Haya mafanikio nimeyapata kutokana na kazi yangu ya muziki, siyo kitu kingine chochote.

“Ndiyo maana natamani sana kuendelea kuishi hapa Kenya kwa sababu ndipo ninapopata heshima na kazi yangu ya muziki niliyoifanya kwa zaidi ya miaka 20 naona inaniweka pazuri,” alisema.

Mr Nice anawaasa wasanii wenzake kuwa wanapopata nafasi, waitumie vizuri na kile wanachofanikiwa nacho wakiendeleze wasibweteke na kitu kimoja, kwani kikitoweka maisha huwa yanabadilika ghafla na kuwa mabaya.

“Unajua mimi ni mwanamuziki, lakini sitakiwi kujiona kuwa kwa kuwa najua muziki, basi ndiyo nifanye muziki kila siku katika maisha yangu

“Uking’ang’ania muziki bila kufanya kitu kingine, utakufa.

“Kwa kukwepa hilo, ndiyo maana nilijiongeza na kuona ni bora hela ninayopata niigawe nifanyie kitu kingine cha kimaendeleo; ndiyo nikabuni mradi wa maji,” alisema.

Mr Nice anaendelea kufunguka kuwa baada ya kuamua kufungua kiwanda hicho cha maji ambacho kimeajiri watu wapatao 30, anakusudia kufungua kiwanda kingine ili tu azidi kujiongezea kipato.

“Nafikiria kufungua kiwanda nyumbani kwa sababu maji yangu hapa Kenya yamekubalika sana, naamini na nyumbani yatakubalika.

“Hakuna kitu kizuri kama kazi yako kuweza kuajiri watu wengine, Nice Water ni bidhaa yangu inayopendwa sana na kuhusu kuileta nyumbani, wala mashabiki zangu wasipate tabu, si muda mrefu nitakuja kutengeneza kiwanda Tanzania.

Mwanamuziki huyo aliongeza kuwa, anashukuru Mungu ameamka na kuweza kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja yaani muziki pamoja na biashara, jambo ambalo analifurahia.

“Mambo haya ya kufanya muziki jukwaani na kujikusanyia mapato, yalikuwa zamani, siku hizi mtindo wa maisha umebadilika.

“Jay Z ni msanii mkubwa duniani mwenye mafanikio makubwa, lakini bado anawekeza kwenye biashara, hategemei muziki peke yake ndiyo maana utajiri wake unaongezeka kila siku.

“Jamaa anamiliki magari ya kifahari na majumba, siyo kwa sababu ya muziki tu bali uwekezaji; hivyo nawaomba na wasanii wengine hasa wa Bongo wabadilike ili kuendana na hali halisi ya maisha ya sasa,” alisema.

Hata hivyo, alitumia nafasi hiyo kuwapongeza baadhi ya wasanii wa Bongo ambao wamejiongeza kimaisha kwa kufanya uwekezaji kwenye sekta nyingine.

Kwa uchache, Mr Nice aliwataja wasanii ambao anawapa tano kuwa ni Mwana FA, AY, Lady Jay Dee, Jacqueline Wolper, Shilole, Diamond ambao alisema mbali na sanaa, wanajituma kwenye kufanya biashara.

“Unaona Diamond anamiliki kituo cha redio na TV, Shilole anafanya biashara ya kuuza chakula,
Mwana FA ana product yake ya manukato, Lady Jaydee alifungua mgahawa, Jacqueline Wolper nasikia kafungua ofisi yake ya ushonaji, hiki ni kitu kizuri ambacho wanafanya.

“Kama nilivyosema, kutegemea sanaa pekee yake ni hatari, mimi nina ushahidi wa kile kilichonikuta kwenye maisha yangu
“Lazima sisi tuwe kioo cha jamii kwa kila kitu yakiwepo maendeleo; tukibaki kufanya jambo moja siku likipotea, heshima itashuka sana.

“Ndiyo maana wasanii wengi wakianguka kisanaa, wanachanganyikiwa kiasi cha kujiingiza kwenye mambo yasiyofaa kama matumizi ya madawa ya kulevya na hivyo kupotea kabisa kimaisha.

“Nimalizie kwa kuwasisitiza wasanii wenzangu tubadilike, tukichezea bahati tutakufa,” alisema Mr Nice ambaye miaka ya nyuma alivuma kimuziki lakini baadaye alichuja na kuanza kuishi maisha ya chini ambayo yaliwasikitisha wengi ambapo kwa sasa ameibuka na mafanikio ya kushangaza.

source

East Africa TV plus+
 
Habari pasi na picha hainogi, hebu tupia kiduchu
habari inasema aliongea kupitia whatsapp, ila Nice namkubali sana , nasikia kuna siku alikuwa bar amekunywa sana bill kama laki 6, muuzaji akamwambia amlipe, jamaa akasema atalipa kwa mpesa akimaliza kunywa, muudumu akaanza kumuwakia na kutoa maneno ya dharau Nice maana aliambiwa na watu nice hana pesa, Nice akachukua simu akamuomba muhudumu namba akatuma zaidi ya laki 6, yani alimuongeza muudumu kama laki hivi akamwambia waitumie kuongeza bia kaunta😂
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom