Blue ni kati ya wasanii tallented kupata kutokea kwenye game ya bongofleva, anauwezo mkubwa wa kurap na kuimba, huyu ni jamii za kina Ngwea. Furaha tele,....tele, wambie wakina... Leo siku ya vigelegele...
Mr umemaliza. Uko sahihi kabisa. Bongofleva wengi ni ama kuimba tu au Kuchana tu lakini Blue kama alivyokuwa Ngwea (R.I.P) anakupa vyote. Iwe ngoma za kibishoo au za kisela kama za BoB micharazo zote anaweza. Yuko vizuri.
Blue ni mfano wa wasanii wachache walioweza kulinda heshima yao kwenye game tangu wanatoka hadi leo, tofauti na wale waliovuma na kushindwa kurudi kushika namba.
Aina ya wasanii walioweza kukamata kitambo na mpaka leo wakishindana na watoto wa sasa ni:
Blue
Fid q
Professor j
Nyandu toz
Joh makin
Kiba
Diamond
Hao ni mfano tu ila wapo wengi waliotamba kwa nyakati zao ila mpaka leo wapo kwenye chati.
Afande Sele aliwahi kuulizwa kuwa kwa nini Blue na Diamond wanajiita simba wakati yeye ndiye anaetambulika kama simba zee, akajibu......wanastahili kujiita hivyo kwa kuwa simba ni mpambanaji na wao wamepambana na kupendwa tangu nyimbo zao za mwanzo mpaka leo wanakamata soko
Ana style za kipeke yake sana. Namkumbuka huyu dogo tangu anaimba freestyle hana hata singo 1.ali washaghairi moto siku moja pale vijana club sio mango balaa. Kulikua na mashindano ya rap.
Ilikua 1999-2000 hivi