chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 21,828
- 29,506
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kimewaita kwenye Kamati ya Kanuni na Maadili wanachama wake 16 kwa kuvunja miiko ya chama hicho kwa kuanza kampeni kabla ya wakati.
Kauli hiyo ilitolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Mpwapwa, Regines John wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kibakwe kwenye vijiji vya Wangi, Nyandu na Lwihomelo Kata ya Wota wakati wa Ziara ya Mbunge wa Jimbohilo, George Simbachawene kutembelea miradi ya umeme inayotekelezwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA).
Alisema uvunjaji wa kanuni unatokana na wananchi kuvunja miiko, kwani sasa watu wameanza kampeni za chinichini za kupita kwa wananchi na kutoa misaada.
Tunakemea mambo hayo kwa mujibu wa kanuni na misaafu ya CCM tayari watu 16 wameitwa kwenye Kamati ya Kanuni na Maadili,¡± alisema na kuwataka wanaotaka kugombea ubunge na udiwani kuwa na subira kwani muda ukifika chama kitaruhusu.
Chanzo: Habari Leo