Kulikua na mama mmoja alikua anatumiwa na international school of tanganyika.Kama mwanafunzi ana matatizo wanampa mzazi contact za huyo mama.Alimsaidia mdogo wangu wa kike[same age] miaka ya nyuma hebu waulize wanaweze kupa contact zake.Tulielekezwa na mtu,mdogo wangu hakusoma pale.
Hebu angalia anatumia simu kiasi gani na internet! Kuna wengine vitu hivi haviwasumbui lakini wengine vinawasumbua sana maana she can meditate on an sms for many hours. Pengine ni ubongo wake tu umekuwa deleted kwa sababu ya psychological problems.
Nasikitika huyo binti kuna vitu ameshavijua, na inawezekana alikuwa akilindwa sana either na wazazi au walezi na sasa kapata upenyo kakutana na maswahibu yaliyomtia kiwewe na kumfanya akili imruke. Ni kama ngómbe wale wanaoitwa wa kizungu, akipata fursa ya kutoka nje ataruka hadi kuvunja miguu huku machozi yakimtoka.
Suggestion:[/u]Mkalishe chini jaribu kumueleza kwamba hivyo vinayomzuzua vipo na havitakwisha, mweleze umuhimu wa elimu katika maisha yake pia mjulishe na mfahamishe kwamba the ONLY RELIABLE MAN (LOVER) IN THIS WORLD IS EDUCATION
Jobo,
Huyu dada hana hata handset ya kubeep. Wazazi wameamua kumweka mbali na mambo ya simu. For now. Kuhusu internet, hapo kwa kweli sijui. Nnachojua ni kuwa hana computer chumbani kwake.
Well, inawezekana kuna ukweli na unachosema. Lakini ni wangapi wanaokutana na maswahibu (like you put it) na bado hawa lose control darasani? Nafikiri amekuwa mzembe tu mwenye. Anahitaji kupelekwa booty camp (joke)
Anatembea na mwalimu wake wa kiume.Muamishe shule au mwambie akutajie ni mwl gani anatembea nae ili uanzie hapo kutatua tatizo hilo.Kuwa shulu ya masista siyo tija sana kwani mambo hayo hufanyika gizani tena KWA SIRI KUU
Post nyingine zinashangaza na kuchekesha kweli kweli....
Ni nini hasa kilichofanya uhitimishe kuwa anatembea na mwalimu wake wa kiume?
Anguko la huyo mtoto from A's to D's na F's wakati hakurushwa kidato siyo rahisi ikawa ni ugumu wa kuingia kidato cha tatu tuu,coz kutoka kidato cha pili hawa-ku-switch ghafla tu na kuanza kufundisha maguuumu.Sasa huyo mzazi/mlezi anasema mtoto ni geti kali na hatoki nyumbani pia shule ni ya masista wakati hapo shuleni kuna walimu wa kiume.Sasa tusemeje kaka.
Majita,
Ni wapi nimesema shule hiyo ina walimu wa kiume? Au unajua ni shule ipi naizungumzia?
Kushuka kutoka A's mpaka D's mbona ni rahisi sana kwa teens. Matokeo ya mpwa wangu yanaweza kuwa yameporomoka kwa ghafla kutokana na moja au mchanganyiko wa sababu zifuatavyo:
1)Daraja la masomo ya level ya Form III limekuwa ngumu kwake kuvuka
2)Amekumbana na mashwahibu mengine (nje ya elimu) ambayo yameiba focus yake ya darasani.
3)Amebadilika na kuwa mvivu, mzembe, na hajali tena elimu.
Na kutokana na 1,2,3 hapo juu, ndio maana najaribu kunyambua tatizo na kulitafutia ufumbuzi.