GE2025 Mpwa wa Hayati Magufuli atinia kugombea ubunge wa Jimbo la Chato Kaskazini

GE2025 Mpwa wa Hayati Magufuli atinia kugombea ubunge wa Jimbo la Chato Kaskazini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera, Venance Stanslaus Martin, ambaye pia ni mpwa wa Hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amechukua fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo la Chato Kaskazini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Venance amefika katika Ofisi za CCM Wilaya ya Chato na kupokelewa na Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Charles Mazuri, na kukabidhiwa rasmi fomu ya kugombea nafasi hiyo ya uwakilishi.

Soma Pia: Uzi maalum wa wanaotia nia kugombea Ubunge Uchaguzi Mkuu 2025

Hatua hiyo imezua mvuto mkubwa kwa wananchi wa Chato na wadau wa siasa, hasa kutokana na historia ya familia yake na mchango mkubwa aliowahi kutoa Hayati Magufuli katika maendeleo ya taifa. Venance anatarajiwa kuwa miongoni mwa wagombea watakaoleta ushindani mkubwa ndani ya CCM kuelekea kura za maoni. Kila la kheri!

Screenshot 2025-06-30 230821.png
 
Kwenye ujasusi ukiona majina yote matatu ni ya kizungu basi unatakiwa kuangalia kwa umakini zaidi.

Zamani nchi ilipokuwa serious hata jeshini hawakuajiri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom