Wakuu suala la elimu kubwa katika kazi halihitajiki. Kinachotakiwa na sifa nilizozitaja hapo juu. Ndo maana nimesema sio lazima mtu awe na cheti cha upishi, n.k.
Ikumbukwe kuwa mpishi Huyu ataajiriwa na kuwa mfanyakazi wa Kampuni na Kwa Hiyo atapata hali zote sawa na wafanyakazi wengine.
Mtu anayetakiwa hapa ni Yule anayejua wajibu wake na kutimiza Majukumu yake bila kufuatwa fuatwa au kusukumwa sukumwa n.k. Kwa Hiyo Naamini sifa hizi watu wengi wanazo. Labda wengine hawapendi "title" Hiyo n.k.
Changamkieni fursa hii. Leo itakuwa mwisho Kwa waombaji na watu watafanyiwa usaili ndani ya siku mbili zijazo. Karibuni.