Mpira wetu wa Tanzania hauwezi kupiga hatua mbele kama kipaumbele chetu ni Imani za kishirikina

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,206
12,747
Naam, wakati real Madrid, Manchester city , wydad Casablanca, Rajacasablanca ,Al ahly n.k, zikipiga hatua kwa kuwekeza pakubwa katika kununua wachezaji nakuboresha mishahara na masilahi ya wachezaji ili wafurahie mazingira wapige kazi hii ni tofauti kabisa na ligi yetu pendwa Nbcpl.

Kipao mbele kwanza Cha timu nikutafuta waganga badala ya kutafuta wachezaji wa viwango, hii ni sumu kubwa kabisa katika maendeleo ya mpira /mpira /timu haitaweza kusonga mbele haswa inapokutana na timu yenye uwekezaji wa hali ya juu.

Mfano maridhawa ni Simba sc kuchoma uwanja pale South Africa nakupelekea timu kupigwa faini kwa kitendo Cha kufanya ushirikina.

Siyo Hilo tu, kitendo Cha basi la timu kuingia uwanjani kinyume nyume. Hizo ni Imani za kishirikina ambapo watendaji wanaamini kuwa tukifanya hivi tutashinda.

Lakini timu Kama rajacasablanca wanapata matokeo mazuri nyumbani na ugenini kwa sababu wame "invest" pakubwa wanawachezaji classic hawawezi kuwaza uchawi/ushirikina wakuchoma uwanja wa mkapa ili wapate matokeo.

Nafikiri mashabiki/wadau wa mpira tuache Imani za kishirikina tuwekeze /tushauri katika kuwekeza pakubwa nakupata wachezaji wenye class Bora katika kudakata kabumbu, hakika ukifanya hivyo hutowaza kuvalisha hirizi wachezaji.

Nimepitia comments nyingi za mashabiki kuelekea derby ya kariako wanawaza uchawi na ushirikina tu.

Mfano

7. Mzigo wa Timu (watu wa mpira na fitna mtakuwa mmeshanielewa) asipewe Mchezaji wa Kigeni na Mkristo bali apewe yule yule Mzawa na Muislamu, ila ajitahidi mno Siku ya Mechi amkwepe sana Bakari Mwanyeto au Farid Musa au Mudathir Yahaya ambao ndiyo huwa Wabeba Mikoba Wao Wakuu." By GENTAMYCINE

Mtazamo/ kipaombele Cha shabiki ni ushirikina kiukweli kwa hali Kama hii mpira wetu utapiga hatua mbili mbele nakurudi hatua Saba nyuma kujipongeza/kujipigia makofi kwa kazi nzuri.

Huwezi kukuta real Madrid, man u arsenal wanachoma uwanja ili washinde mechi hakuna kitu Kama hicho, sajili wekeza vizuri uone kama hutopata ushindi.
 
HAKIKA UMENENA VYEMA,. MKOMBOZI WA FIKRA KATIKA JUKWAA HILI PENDWA.
Asante sana mkuu kwa kunitunuku jina la "mkombozi wa fikra" hakika umetia moyo katika harakati zangu za kuleta mabadiliko.

Najua Kuna watu watakuja kutoa povu hapa.
 
Naam, wakati real Madrid, Manchester city , wydad Casablanca, Rajacasablanca ,Al ahly n.k, zikipiga hatua kwa kuwekeza pakubwa katika kununua wachezaji nakuboresha mishahara na masilahi ya wachezaji ili wafurahie mazingira wapige kazi hii ni tofauti kabisa na ligi yetu pendwa Nbcpl...
Ahahahaaa

Naona Leo umeamua kumnyoosha mtani wangu GENTAMYCINE
 
Soka letu kivyetu vyetu huo ni utamaduni wetu mtuache na sio uchawi huo
Kama ni utamaduni wenu basi tunaomba huu utamaduni ubaki kwenu na siyo kwenda kulidharirisha taifa kwa kuchoma uwanja wa wenzenu.

Alahly walikuja hapa uliona wamechoma uwanja?
Raja walikuja huku uliona wamechoma uwanja??

Hebu huo utamaduni wenu badilikeni.
 
Gentamacimavi ndio mtu unaleta upuuzi wa ushirina humu jamvini.

Jukwaa limekuwa la kipuuzi namkumbuka nguli wa Abajalo Sinza Gang Chomba sijui amepotelea wapi, jukwaa limepwaya sana.
 
Kama ni utamaduni wenu basi tunaomba huu utamaduni ubaki kwenu na siyo kwenda kulidharirisha taifa kwa kuchoma uwanja wa wenzenu.

Alahly walikuja hapa uliona wamechoma uwanja?
Raja walikuja huku uliona wamechoma uwanja??

Hebu huo utamaduni wenu badilikeni.
Na wao wanayo ya kivyao usiyaona kwa macho.Usikariri mzee wa mwiko.
 
Back
Top Bottom