Mpinga maendeleo hana tofauti na mpinga Kristo

Maramla

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
581
642
Kumekuwa na kelele nyingi zinazohusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa Nchini, awali vigezo vya kupingwa maendeleo ilikuwa "SERIKALI INAFANYA MIRADI ISIYOSAIDIA WATU WOTE".

Ununuzi wa ndege ulipingwa, ujenzi wa reli ulipingwa, mradi wa bwawa la kufua umeme ulipingwa hata elimu bila malipo ilipingwa.

Baada ya Mhe. Rais Magufuli na Serikali kukaza msuli na kuonesha matokeo chanya, wale wote waliopinga miradi hii kutekelezwa wamehamishia hasira zao Chato.

Kwanza nawapa pole sana kwakuwa maendeleo hayataweza kusimama kwakuwa mpinga maendeleo anapiga yowe.

Kwa wanaosoma maandiko matakatifu watakubaliana nami kuwa Yesu alipingwa alipoponya, alipofufua, alipofundisha pia. Mwisho walihamishia hasira zao kwenye uhai wake, lakini neno halikukoma.

Hivyo nchi itaendelea kusonga mbele na hata Msipoisema Chato basi mtaisema Tandahimba.
 
Mambo ya imani yanaingiliana vipi na siasa? Yesu aliwahi kujenga wapi madaraja au kununua Bombardier hapa duniani?

Mambo ya Kaisari usiyachanganye na ya Mungu, kama unaona sahihi kila mradi kupelekwa Chato utakuwa na matatizo ya akili.

Nawasubiri kesho mtuambie Yesu akirudi duniani atateremkia Chato.
 
Naona hoja zimeshindikana kujibika juu ya miradi kuelekezwa Chato! Mnakuja na version tofauti tofauti lakini bado ni porojo tu!
Tafuteni watu wenye akili timamu huko wawasaidie kujibu kitaalamu hoja zilizoko mezani!

Daaah eti Taifa Stars Vs The Cranes, uwanja ni Chato international stadium!!😁😁😁😁
Tutafika tu!
 
Mtaibuka Sana wanufaika but ni Kodi zetu,mnaangalia njaa zenu tu na huruma ya Kodi zetu,pindi yatakapogeuka magofu
 
Mambo ya imani yanaingiliana vipi na siasa? Yesu aliwahi kujenga wapi madaraja au kununua Bombardier hapa duniani?....

Kwani Chato hamna watanzania? Halafu hiyo miradi ya maji nchi nzima, vituo vya afya, maboresho ya uwanja wa Songea, ile hospitali ya Kanda Mtwara, Ile hospital ya Nyerere Musoma, Hospitali za mikoa zinazojengwa je?

Au huko nako mmepabaitiza CHATO? Mwisho wa Siku wote ninyi hamna tofauti na mpinga Kristu...ila neno halitakoma.
 
Hata Mobutu alikua na Chato yake lakini alipogeuka mzoga mambo yakawa Hivi
IMG_20210114_113028.jpg
IMG_20210114_112758.jpg
 
Kinachotakiwa ni maendeleo ya watu na si maendeleo ya vitu, maendelea ya vitu hayana maana kama watu wako wanabakia kwenye lindi la umaskini, afya mbovu, elimu mbovu huku wakiwa wamejaa woga na kutojiamini
 
n
Naona hoja zimeshindikana kujibika juu ya miradi kuelekezwa Chato!Mnakuja na version tofauti tofauti lakini bado ni porojo tu!
Tafuteni watu wenye akili timamu huko wawasaidie kujibu kitaalamu hoja zilizoko mezani!

Daaah eti Taifa Stars Vs The Cranes,uwanja ni Chato international stadium!!!!😁😁😁😁
Tutafika tuuu!
Mimi namba shirika la nyumba la taifa lihesabu wana chato wote, nyumba za bei nafuu zijengwe ili kila familia imiliki nyumba - tunataka CHATO liwe jiji la mfano Afrika - hutaki basi saga unwe viwembe
 
Mleta hoja una tabia ya kukurupuka mno utafikiri uharo! mbona hujui kuandika kwa mpangilio na kujenga hoja?
This is rubbish!
Najua kwako wewe mtu Mwelevu ni yule anayepotosha, kuogopesha, mwenye husda na chuki.
Kwahiyo mimi nawewe hatuwezi pimwa kwa mizani moja kwakuwa una jicho la kobe... Yaani banda lako unatembeanalo mgongoni.
 
Kinachotakiwa ni maendeleo ya watu na si maendeleo ya vitu, maendelea ya vitu hayana maana kama watu wako wanabakia kwenye lindi la umaskini, afya mbovu, elimu mbovu huku wakiwa wamejaa woga na kutojiamini
Mtazame huyu!!!
Vitu hujenga watu na maendeleo Yao, na ndio maana unaona miradi ya afya, barabara, usafiri wa anga, usafiri wa majini na miradi mingine ikiwemo umeme inatekelezwa kwa kasi ili kurahisisha maendeleo ya watu.
 
n
Mimi namba shirika la nyumba la taifa lihesabu wana chato wote, nyumba za bei nafuu zijengwe ili kila familia imiliki nyumba - tunataka CHATO liwe jiji la mfano Afrika - hutaki basi saga unwe viwembe
Ni sawa kwa mtu mwenye akili finyu kama wewe!
Maneno ya kanga ni dalili ya kutopevuka!Mtu smart,timamu na aliyekomaa hawezi kutokwa na maneno ya rejareja kama wewe!
Subiri wa level yako ndio mtafanya nao mjadala,sio mimi!
 
Jamaa acha upumbavu... kwani chato hamna watanzania? Halafu hiyo miradi ya maji nchi nzima, vituo vya afya, maboresho ya uwanja wa Songea, ile hospitali ya Kanda Mtwara, Ile hospital ya Nyerere Musoma, Hospitali za mikoa zinazojengwa je? Au huko nako mmepabaitiza CHATO? Mwisho wa Siku wote ninyi hamna tofauti na mpinga Kristu...ila neno halitakoma.
Unamjengea nani uwanja wa ndege kijijini? au ndio hao watalii tulioambiwa jana watakuwa wanakuja kuangalia amani ya Tanzania inayopatikana Chato?!

Nyie jinga sana.
 
Tatizo hata hao viongozi wamepatikana kwa njia gani,, na hayo maendeleo yatakuja kweli,, kwasababu kila kitu kikiwa haramu hata maendeleo yatakuwa haramu tuuuu
 
Maendeleo ni kuzalisha mali,Kama unavyoona vitu Kama Tecno,samsung,air-condition,magari ya toyota,nissan,bettry,hivi vitu vikizalishwa ndio maendeleo,sasa wewe unaenda kujenga Ikulu Dodoma,hostel ya Waziri mkuu,wakati Dodoma,Ikulu ndogo ipo,makazi ya Waziri mkuu yapo,sasa hayo maikulu yaaningiza Tsh ngapi?

Sisi hatupingi Chato kujengwa stendi ya daladala,hospitali,au chuo Cha veta,hivi ni vitu vidogo sana,ni huduma kwa jamii,unapoenda kujenga Airport ya mabilioni ya pesa Kama ya Dar,wewe unaijenga Chato!hivi kwa mwaka uliopita Chato imechangia Tsh ngapi,kwenye pato la Taifa?

Unaacha kujenga au kupanua airport ya Arusha,unaenda kujenga Airport ya mabilioni,songwe,au Masasi,au Tunduru,
We utakuwa na akili kweli?
 
Vipi mmejenga kwa pesa ya ndani, maana hivi karibuni nimeona kujikombakomba sana kwa mchina...
 
Ni sawa kwa mtu mwenye akili finyu kama wewe!
Maneno ya kanga ni dalili ya kutopevuka!Mtu smart,timamu na aliyekomaa hawezi kutokwa na maneno ya rejareja kama wewe!
Subiri wa level yako ndio mtafanya nao mjadala,sio mimi!
Si maneno wala mtazamo wangu lah hasha bali ni maneno na mtazamo wa chama tawala kinachokuongoza ukiwemo na wewe kwamba priority leo ni chato !! Nothing u can do my friend!!
 
Back
Top Bottom