Mpina: Hatumuogopi Rais Magufuli

Mpina: Hatumuogopi Rais Magufuli

Azim Sokoine

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2014
Posts
1,485
Reaction score
2,752
Zile hisia zilizozagaa mitaani kwamba mawaziri wamekuwa wakitekeleza majukumu yao huku wanamuogopa Rais John Magufuli imepata jibu.

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhaga Mpina amesema wakichukua hatua stahiki dhidi ya watendaji wanaokiuka maadili ya utumishi wa umma hivyo siyo kweli kuwa wanaogopa kumshauri Rais Magufuli.

Akihutubia mkutano wa hadhara kijijini Mwandoya wilayani Meatu, Mpina amesema baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakibeza utendaji wa baraza la mawaziri wakidai ni waoga wa kumkosoa hata kumshauri Rais.

“Wenzetu wa upande wa pili ambao ni wapinzani wamekuwa wakitubeza mawaziri tulioteuliwa na Rais Magufuli kuwa tumekuwa waoga, hivyo kushindwa kumshauri na kulifanya Taifa kusinyaa. Haya siyo ya kweli, ninyi ni mashahidi mmeona jinsi tunavyochapa kazi,” amesema Mpina.

Mpina ambaye ni Mbunge wa Kisesa wilayani Meatu, amesema wataendelea kuwachukulia hatua viongozi wa Serikali bila ubaguzi wala kumuonea mtu na watafanya kazi wakitekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.

Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Meatu, Juma Mwiguli ametaka Rais Magufuli aongeze kasi ya kusafisha viongozi wabovu walioko madarakani akidai ndiyo waliolifikisha Taifa lilipo kutokana na kushamiri ubadhirifu wa mali za umma.


Chanzo: Mwananchi
 
Umeonge tumemsikia, nihiayari yetu kuamini maneno aliyozungumza au vinginevyo. Tunaona na tunasikia pia.
 
Naibu Waziri anakutana wapi na Rais?? Thubutu yake!! Mawaziri wenyewe wanaomba appointment na lazima uwe na cha maana na inakuwa story kabisa kuandikwa press release! Mpina atulie tu! Asilete siasa hapo!! Hata barazani haingii anasikia story tu!!
 
Back
Top Bottom