Mpiganaji asiyeshindwa Vita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpiganaji asiyeshindwa Vita

Discussion in 'Sports' started by Anselm, Aug 15, 2012.

 1. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Wakati niliposoma tambo za Msemaji(ovyo) wa team ya Simba kuhusiana na usajili wa Ngassa na Twite Simba na baadaye kusikia kashfa alizozitoa Mwenyekiti wa Club hiyo dhidi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Yanga "Mpiganaji" Abdalah Binkleb,niliamini 1 kati ya mambo mawili juu ya viongozi hao,Walikuwa hawajui wanachokiongea au walikuwa wanaendeleza kile kilichogundulika ndo silaha yao kubwa ya kuwapumbaza Wanachama wao cha "kubwabwaja ovyo".
  Abdalah Binkleb kwangu mimi mpaka muda huu ni Mpiganaji asiyeshindwa vita.
  Baada ya kushinda vita dhidi ya APR msimu uliopita iliyohusisha usajili wa moja ya Middle za ukweli katika bara hili Haruna Niyonzima "Febregus" niliamini Rage,Kaburu na Baba yao Zacharia Hanspop wasingeweza kushindana na Kijana huyu pale ambapo ataamua.
  Ni mmoja kati ya Wafanyabiashara wasomi wanaoendesha mambo yao kisomi,mkimya na asiyependa kuongea sana na vyombo vya habari,siku zote anajua anachokifanya na ndo maana tumekuwa tukijipatia nafasi ya kushuhudia ushahidi usio na shaka kama hivi (tujikumbushe):-
  niyonzima 2.JPG
  Baada ya kushinda vita dhidi ya team ya familia ya Rais wa Rwanda,Binkleb alimkabidhi jezi Haruna Niyonzima hii ilikuwa ni mwanzoni mwa msimu wa mwaka jana.

  Kama hiyo haitoshi baada ya kashfa,akawafanyia hiki;-
  jersey.jpg
  Hivi kweli jamani ashindwe Alex Kagame(Mdogo wake wa damu na Rais Kagame wa Rwanda) aje kuweza Rage?
  Vita iliyoanzishwa na tambo na kashfa za kijinga ikamalizika kwa style hii.

  Pamoja naye kuna vichwa vingine vinavyoshirikiana naye katika kuitengeneza Yanga imara itakayokuwa katika level nyingine kabisa:-
  Kelvin.jpg
  Huyu anaitwa Seif Magari,mmoja wa Viongozi wa Kamati ya usajili ya Yanga waliofanikisha ushindi wa 5-0 wa nje ya uwanja ukijumlishia na usajili wa Said Bahanuzi ambaye habari zinathibitisha kwamba alitolewa Mtibwa kuelekea Msimbazi lkn hapa katikati Wajanja wakamkwapua na kumwelekezea Jangwani,na Aly Mustafa Barthez ambaye alikuwa bado kwenye mipango ya Simba.
  Hapa baada ya kumaliza kazi,alikuwa akimkabidhi jezi Kelvin Yondan "Vidic"
   
 2. m

  makumvi Member

  #2
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 26, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa Niyonzima alilamba dume, lakini kwa Yondani na Twite nadhan tusubiri kwanza maana game bado halijaisha kujua nani mshindi.
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Hovyooooooooooooo! Hii ni kwa bongo tu ndo usajili ni wa kihuni
   
 4. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  mwenye akili timamu sidhani kama anaweza kujivunia kwa vitendo vya kiuni vinavyofanywa na Yanga kuiujumu Simba hususani ktk hizi harakati za usajiri; Yanga semeni tu kama vipi tuwakabizi kikosi kizima cha Simba kwani kila kukicha mnakitolea macho, alafu tuone mtashindana na nani.
   
Loading...