Habari za leo ndugu wana MMU,
Ni karibu miezi nane imeishatoka tulipoachana na mpenzi wangu kutokana na sababu mbalimbali hasa mimi nikiwa ndio chanzo cha sababu hizo.
Tumekuwa tukiendelea kuwasiliana na huyu x wangu na mara zote alionesha hali ya kutaka turudiane. Lakini tayari mimi sikuwa na mapenzi tena kwake kama zamani.
Sasa leo kanitumia meseji na kunieleza kuwa keshokutwa kutakuwa na sherehe kwao ambapo mchumba wake atapeleka mahari pamoja na kumvisha pete ya uchumba. Amenisistiza sana uwepo wangu kwani baada ya kuachana hatukugombana tena na wala hakuna mwenye kinyongo juu ya mwenzaje.
Na hata kipindi cha hivi karibuni aliniomba nimruhusu kukubali mchumba mwingine kama mimi sipo tayari kumuoa, na mimi ni kamwambia poa wewe ukipata mwingine sawa endelea nae tu.
Naombeni ushauri kwa wazoefu vipi hii imekaaje? Je nikienda haitaweza kuleta madhara?
Karibuni kwa michango yenu