Mpenzi wangu anataka nifuge Rasta

Hahahaaaa kwan wew hupendi rasta looo!!!

Tatizo wala sio rasta ila hivyo vijisharti vyake sasa kama anawazimikia marastafari si shida hiyo na ninawasiwasi huyo demu atakuwa alionjeshwa cha Arusha na huyo rasta wake wa mwanzo ndo mana akili zake zipo hivyo.,
 

Acha kuebdeshwa na skteti.Mwache asepe akawatafute marasta
 
Drama Queen with another Episode. ..what next..?
 
kuwa na msimamo.....itakuwa kama ninataka me au ke mnene...wha if akikonda je........
 
Kesho atakwambia uchore tatoo yenye jina lake, siku nyingine unyoe upara ilimradi akupeleke peleke, btw, mtu anaehamisha kukumbukumbu za ex wake kwenye mahusiano mapya ni tatizo.
 
Aisee mkuu makolola, pole sana kwa kutokuwa na mwenza bali unakiwiliwili chake tu na moyo wake haupo kwako! Anasema umeuponyesha moyo wake wakati anakiri mpaka sasa hana furaha mpaka pale utakaposuka rasta kama bwana wake? For sure mpaka sasa unaye huyo mwanamke kwa sababu anahitaji kampani tu baada ya kuachwa na jamaa hivyo kuji-feel mpweke! Najua mpaka sasa hana uhakika kama anakupenda! Think out the box and be a man!

Aisee mkuu Kozo Okamoto umemaliza kabisa kile nilichokuwa nimekiona kwenye kisa cha jamaa yetu! Huo ndio ukweli!
 
Last edited by a moderator:
Usifanye chochote kile ambacho wewe mwenyewe hukipendi ili kumridhisha mtu mwingine hata kama ni MUPENZI.
Niko pamoja na wewe mdau....Life's hard. It's even harder when you're stupid #just saying
 
Tatizo wala sio rasta ila hivyo vijisharti vyake sasa kama anawazimikia marastafari si shida hiyo na ninawasiwasi huyo demu atakuwa alionjeshwa cha Arusha na huyo rasta wake wa mwanzo ndo mana akili zake zipo hivyo.,

hahahaaaaa looo
 
Wewe kuwa mwamuzi wa mwisho na kwa kuongezea kitu ambacho hujisikii usijilazimishe eti kwasababu ya kumridhisha mtu mwingine hapana, kataa.

Nakupa kisa cha ukweli kilichonitokea kuna demu mmoja kipindi tulipokuwa marafiki(wapenzi) alikuwa ananilazimisha nitoge masikio mawili nikamkatalia, akaniambia toga japo moja nikamkatalia akaniambia "iwapo wewe unanipenda kweli kwanini hutaki kufuata kinachonipendezea mimi?" mimi nikamjibu sitoweza kwa kweli akendelea kuniambia "iwapo sitafafanya anakavyotaka mimi na yeye itakuwa basi" nikamjibu kwa roho nyepesi ruksa, baadae akatulia na mimi sikufuata sharti lake na ikafikia hadi siku ya yeye na mimi kumalizana kwa usalama.

Unajua kwanini nimeleta kisa hiki? Unafikiri ingekuwaje iwapo ningemfuatisha demu kutoga masikio na baadae mnakuwa hampo pamoja tena. Wewe huoni ni upumbavu wa hali ya juu.

Tunapokuwa tunaleta mifano hai kama hii huwa tunataka mjifunze, tatizo wengine wanakuwa hawaelewi unapoweka kisa kilichokutokea ili kwa mwenye ufahamu apate kujifunza jambo
 
Ukikubali tu we boya.

Anachomaanisha ni kwamba bado anampenda huyo jamaa ila hana namna so ili ajihisi yuko naye basi wewe uwe mdori wa huyo jamaa kwa kufuga rasta.
 
Heheeeee! Mahaba nyenyekevu hayo!!!
Mwambie asimtafute X wake ndani yako maana hatompata,wewe ni wewe na X abaki kuwa X.
Achague kukukubali ulivyo au arudi akambembeleze X warudiane,ukikubali rasta zikikua atakwambia uanze kutembea na vibegi mgongoni!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…