Mpenzi wake amechukua fani ya Engineer, na anaogopa atakuwa mchafu

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
7,906
10,759
Wandugu ebu munipe njia nimtie moyo huyu rafiki yangu hajitambui wala hana raha kabisaa.

Rafiki yangu huyu alichumbia mchumba tangu huyo mchumba akiwa form five, sasa huyo mchumba anasoma masomo ya Engeneer na anaona kama amepoteza matarajiao yake.

Mara ya kwanza alijua mchumba wake atasomea udakatari or phamacy. Ila kwa sasa ndio hivyo anasoma Engeneer na nimejitahidi sana kumshauri lakini hataki kusikia japo analia sana kwa vile anampenda sana binti hakuwa na mpango wa kumuacha alikini sasa ndo ivo tena.

Hoja yake iko sehemu hii.
1. Mke Engeneer hawezi kuwa nadhifu hata siku moja.
2. Atamuacha na kusafiri kila mara huku yeye akilea watoto
3.Hataweza kushiriki kikamilifu katika familia kwa ubize wa kazi zake

Sasa wanajamvi wazoefu ebu munipe nondozi za uzoefu nikamshauri huyu rafiki kabla hajafika mbali .

Angalizo, ushauri huo usije ukaniumbua mimi baadae.

Karibuni.
 
Ooh poor me kumbe ndio jamii inavyowaona wanawake wanaofanya kazi hizo?mama yangu ni fundi magari gereji moja kubwa,na amekua mrembo na msafi siku zote,tumekua vizuri na kwa heshima,usahi na unadhifu ni hulka ya mtu.wapo maprofesa nani rafu kweli
 
Sasa angeolewa daktari ingekuwaje.mimi nimeolewa na nahayo unayoyasema sijaona.kifupi ni watu wasiokuwa na maneno mengi au longolongo,hawaigizi maisha,watafutaji,siwatu wa macho mia mia,akipenda amependa wala hatanii.Inawezekana sio wote lakini wale ninao wajua
 
Acha kudhalilisha professional yangu aiseeee.....
Me Mechanical Engineer, nimekua fully smart na kula kiyoyozi 24/7, tena kwenye nchi za hao wanaojisema wame endelea. Daily naingia meeting nafanya bla..blaaahh... na vingereza vingiiiii....., mwisho wa siku napokea report ya yalio jiri.
Then kwa fani hiyo hiyo nimekua CEO kwa my own company huko Bongo, na nimetoa ajira kwa watanganyika wenzangu zaidi ya 25
 
Sasa angeolewa daktari ingekuwaje.mimi nimeolewa na nahayo unayoyasema sijaona.kifupi ni watu wasiokuwa na maneno mengi au longolongo,hawaigizi maisha,watafutaji,siwatu wa macho mia mia,akipenda amependa wala hatanii.Inawezekana sio wote lakini wale ninao wajua

Hureeee....;);)
Nafuu umenipoza mtima mkuu, maana huyu mleta uzi imenifanya nitoe povu mbaya aiseeee....
 
Yeye kama anaona ataumia mbeleni yanini kuendelea kung'ang'ana na kitu ambacho kitakuja kumletea madhara.
 
Usafi ni tabia kutoka utoto,wewe kama engineer alaf mchaf bas hiyo ni tabia yako ya uchaf umekua nayo.

Kikubwa ni tabia, profession ya mtu sio kigezo,mbona madaktar wanavaa nguo fup mapaja nje husem?

Kama unataka wa kuangalia family oa mwalim kwan mwalmu anamaadil kwa nyanja,uvaaji,tabia nk.

Kikubwa kama wamependana hakuna shida yoyote achana na dhana ya kusema engineer wachafu "TUTAKE RADHI"

kuna mdau hapo juu amesema mama yake anafanya kaz garage lakin msafi

hivyo ucje kuona mtu kweny gar nazile jez zake za kaz bas ukasema mafund magar wote wachafu,
utakuwa umepotosha uma mazima ,hiyo ni tabia yake tu amekua nayo.
 
Mawazo ya wavulana, mshauri awatafute wanakamati ya mashindano ya ulimbwende watamsaidia.
 
Usafi ni tabia kutoka utoto,wewe kama engineer alaf mchaf bas hiyo ni tabia yako ya uchaf umekua nayo.

Kikubwa ni tabia, profession ya mtu sio kigezo,mbona madaktar wanavaa nguo fup mapaja nje husem?

Kama unataka wa kuangalia family oa mwalim kwan mwalmu anamaadil kwa nyanja,uvaaji,tabia nk.

Kikubwa kama wamependana hakuna shida yoyote achana na dhana ya kusema engineer wachafu "TUTAKE RADHI"

kuna mdau hapo juu amesema mama yake anafanya kaz garage lakin msafi

hivyo ucje kuona mtu kweny gar nazile jez zake za kaz bas ukasema mafund magar wote wachafu,
utakuwa umepotosha uma mazima ,hiyo ni tabia yake tu amekua nayo.
Samahani mkuu, ndo maana nikaleta hapa ili nipate nondo na kuwaelimisha wengine pia. hii ni kuwafumbua watu macho kama ulivoshauri, asante
 
Back
Top Bottom