Mpenzi wa zamani anataka kuniharibia ndoa yangu

Mpenzi wa zamani anataka kuniharibia ndoa yangu

Mtetezi.com

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
3,134
Reaction score
3,601
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza,

Niende tu moja kwa moja huenda nikapata hata mwongozo wa kimawazo kwani kisaikolojia tumeaminishwa yakuwa ukiwa na tatizo/changamoto ukimweleza mwenzeko/mwingine ni nusu ya kutatua tatizo hilo.

Katika harakati za maisha nikiri tu niliwahi kuwa na wapenzi tofautitofauti na huyu ninayemzunguzia tulikuwa naye chuo baada ya pale hatukuachana ila tulitengana kutokana na harakati za kutafuta maisha na baada ya muda tukapotezeana mawasiliano kabisa kwani mimi nilibahatika kwenda nje ya nchi.

Namshukuru Mungu baada ya miaka miwili nilikitimiza kilichonipeleka huko nikarejea na miaka mitano iliyopita nikabahatika kukutana kazini na binti mmoja mrembo sana na nikamuoa na maisha yakaendelea.

November mwaka jana nilipokea facebook messege kutoka kwa yule mpenzi wangu wa chuo ikisema "Dunia tunapita mengi ila yakipita tunayaacha na kuyasahau" Baada ya ujumbe huo nilitafakari ila sikuujibu ila siku zilivyozidi alikuwa akinisalimu kila kukicha na mimi nikajikuta napokea salamu kwani niliamini ni lengo tu la kunijulia khali kumbe ana lake kichwani.

Ghafla tukajikuta tumekuwa marafiki wa kawaida tunachati, kutumiana picha ghafla akataka eti kukumbushia na anajua nina mke hapo ndipo zahama ilipoanza kwa baada ya kuniambia amenimiss na anajua nimeoa lakini hajali kwani yeye ni kabla ya aliyeolewa hivyo hamwogopi kwa lolote na bado ananipenda na hatujaachana.

Nilichoamua kufanya nilimuomba tuonane ila sio siri hata mm sikuwahi kumwacha ila tulitengana tu hivyo na mimi bado nina hisia naye sana japo nikajikaza kidume asijue na shetani asinizidi.

Akaomba tukutane weekend nikakubali kwani kumbe yupo hapa hapa town nikasema sawa tulipokutana duh Mashaalah amependeza sana yani ameiva kinyama yupo tayari tu kuliwa huku nikiangalia wowowo sio siri taarabu imo nikasema isiwe kesi kufa kwa kiu baharini ni uzembe na kwakuwa alishaniambia jiskie "huru kwa chiochote" nikamchomekea kuwa "salama lakini"? Akasema kama huniamini twende tukacheki.

Tumeenda kucheki wote tumenusurika Alhamdulillah na baada ya hapo tukala tunda lile lililomponza baba yetu Adam sasa sijui tuseme amenogewa au anataka kurejesha koloni lake mana amekuwa ni msumbufu hatari kila siku anataka na kila mara text kiasi ya kwamba mama watoto ashaanza mashaka na namba yake kashaisave.


Kumpenda nampenda, mke wangu nampenda, ndoa yangu naipenda nifanye nini wadau?
 
Mtu hujaribiwa na Tamaa yake..huoni tayari umeharibu kutembea nae? Ndoa hutengwa na uzinzi na kifo! Hapo ushatimiza kifo cha ndoa. Muombe msamaha mkeo. ..vinginevyo waoe wote kama imani inaruhusu.
Akipandacho mtu ndicho huvuna.
 
Huo n udhaifu Mkubwa ukiachana na mtu haitakiwi kurudiana na pia hata mazoea nae hayatakiw kabsa
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Huo n udhaifu Mkubwa ukiachana na mtu haitakiwi kurudiana na pia hata mazoea nae hayatakiw kabsa..maana always mwsho wake unakuaga kurudia mech mwshowe upate majanga bureeeeee
 
Back
Top Bottom