The Donchop
JF-Expert Member
- Jan 10, 2014
- 294
- 378
Habari zenu wanajamii forum,
Nimepata mpenzi ambaye hatuna muda mrefu, amekuwa muwazi kwangu nami nimekuwa open kwake. Amenieleza kuwa ana mtoto ingawa haiwezekani yeye kuoa huyo mzazi mwenzie kutokana na kuwa ilitokea kwa bahati mbaya.
Hakuwa na plan ya kuzaa na binti huyo. Na walipojaribu kuitoa mimba hiyo pia ilishindikana kutoka na sababu za kiafya za binti. Hivyo ana mtoto lakini haiwezekani kuendeleza mahusiano na binti.
Baada ya uwazi huo, nilikubali kuwa naye. Kinachonipa wasiwasi ni jinsi ukaribu huo na mzazi mwenzie unavyozidi. Haiwezi kupita siku bila kuwasiliana kwa kupigiana au hata kutumiana messages.
Nimejaribu kuongea naye kuhusu ukaribu huo unavyoniletea mashaka, mwenzangu ameniambia kuwa ni maongezi ya kawaida tu. Inawa sijaridhika na majibu yake.
Napenda kufahamu wanajamii,inawezekana kweli mtu na mzazi mwenziwe wakaachana kweli ama ni mimi nimeingilia mapenzi ya watu! Nipo njia panda. Sielewi nichukue maamuzi gani mpaka sasa.
Naombeni mnishauri wanajamii.