Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,374
- 38,248
[SUB]Basi tukakaa kila mtu na siti yake, pembeni yangu ni John, kijana mtaalamu wa Mechanics, uzoefu wa gereji za katikati ya jiji la Kampala, siti mbili za mbele yetu walikaa Milgo na Fatma, mabinti wa Kisomali, kwa walivokaa katika zile siti ni sawa na kusema Milgo alikaa mbele yangu na Fatma alikaa mbele ya John.
Kilichokuja kujulikana baadae ni kwamba, Milgo ni mfamasia kitaaluma na kwamba elimu hii aliipatia Kenya, nchi ambayo walihamia na kuweka makazi yao, kitambo baada ya wazazi wao kukimbia machafuko Somalia. Kwao wao ni raia wa Kenya, hawakubali kwamba wao ni Wasomali nililijua hilo.[/SUB]
[SUB]Wao kwa wao niliwaskia wakiongea kitu ambacho baadae niliamini ni lugha yao ya asili, Kisomali. Kuna wakati walikuwa kama wamenogewa na story zao, waliongea Kiingereza, bahati nzuri kwangu, lugha hii iliokuja kwa Meli, siwezi kuiongea, ila naweza kuisikiliza vizuri, nikatumia uwezo wangu wote kujua na kuwaelewa wanachoongea, nikafanikiwa.
[/SUB]
[SUB]Uzuri wa mabinti hawa wa Kisomali, nahitaji 1Tb ya Hard disk ili kuuelezea hapa. Ni wazuri naomba utosheke na maneno hayo kuwa ni wazuri. Kama utataka kuthibitisha uwezo wa juu kabisa wa Muumbaji, hapa kwa mabinti wa Kisomali ilikuwa ni moja ya ushahidi huo. Mara nyingi huwa tunaaminishwa kuwa vazi la buibui ni moja ya stara kwa mwanamke.
Kwa kuwa huficha maungo yake, haikuwa hivo kwa Milgo na Fatma, hawa hata wangejifunika turubai la Canvas ya Morogoro, bado ungejua tu kwamba, viumbe hawa wamebarikiwa, sio wale wenzangu na mie waenda mbele kama wanarudi, kwa haraka haraka hujui mbele wapi na nyuma wapi.[/SUB][SUB]Hawa wamebarikiwa![/SUB]
[SUB]Milgo alikuwa na yale macho ambayo wenzangu na mimi ukitazamwa mara moja tu na binti, unawahi kuingiza mkono mfukoni ili kuweka sawa mambo, yaani unaokoa jahazi lisizame, sio hela! Kama hujawahi kuona mkia wa farasi, ningekusaidia kukuonyesha nywele za Milgo zilivomwagika nyuma ya kichwa chake, afu ningekuambia huo ni mfano tuu!
Kwa aile sura yake, nna uhakika amepitisha muda mwingi sana tangu mara ya mwisho aliponuna, na huenda ameshasahau kununa kukoje![/SUB][SUB] Milgo akikutazama ni kama anakuita mototo wa kiume, macho yake yana kila dalili ya kumuonea huruma Mwanaume, sura yake iliobeba macho yale, akutazamapo ni sawa na mdada anaemtazama mpenzi wake aambae anafunguliwa mlango wa jela, na kuruhusiwa kutoka baada ya kifungo cha miaka dahali.
Huku mdada akiwa na ushahidi usio na shaka yeyote kuwa, mpenzi ana ukame, kibuyu kimejaa zaidi ya maana ya neon kujaa![/SUB][SUB]Kwa kifupi Milgo alishanimaliza.[/SUB][SUB]Alinimaliza pasi na yeye kujua. [/SUB][SUB]Moyoni mwangu kulikuwa na mnyukano mkali. Ningekuwa wa kike ningesema, mnyukano huu ni matokeo ya KITCHEN PARTY, mnyukano uliosababishwa na watu wangu wa karibu na nafsi yangu. Watu wangu wa nyumbani walishanikaririsha kuwa MSAFIRI, msemo huu niliukariri kwa muda mrefu sana, leo ndio najione.
Wakaenda mbali zaidi kuwa, nahitaji kuwa makini safarini, na hasa katika safari za masafa marefu kama hii. Wakanisihi kuzidisha umakini ndani ya chombo cha usafiri, wakasema niwe makini na kila abiria wa karibu yangu. Wakasema niwe makini na nizidishe sana dua hasa katika miji mikubwa ntakayopita.
MSAFIRI, wakasema nisilale, niwe macho, hasa nyakati za usiku, tena zaidi katika miji mikubwa ntakayopita na basi, wakasema kuna Mafia wa kutosha Lusaka, niwe makani. Pia nikaambiwa niwe macho kama itatokea nikaingia Harare mida ya Usiku, ni kama Jehanamu ndogo!
Na kisha wakanambia nisikae kiboya boya Johannesburg, na tena kama itakuwa Usiku![/SUB][SUB] Homeboy wangu alienisindikiza mpaka Ubungo terminal, yeye aliniasa kuwa mbali na watoto wa kike kipindi chote cha safari, na hasa kama ntakutana na msichana mrembo, anasema hawa ndio wanaotumika sana katika vitendo vya Kimafia na ikibidi kupoteza uhai kama si kupoteza vile ulivonavo msafiri![/SUB]
[SUB]Wakati huu ambao tayari akili na moyo vinabishana, vinavutana kuhusu hiki kiumbe cha kike, mbele yangu, Milgo nasaha zote nilizokuwa napewa na watu wema mbali mbali waliokuwa wanantakia mafanikio katika safari yangu na maisha mapya ntakayoyakuta Cape town, zikawa zinapita kichwani moja baada ya nyingine, huku sura za wasemaji nazo zikinijia! [/SUB]
[SUB]Mpaka sasa akili yangu haikubali kuwa naweza nikaanzisha mchakato wowote wenye dhamira ya mapenzi kwa Milgo, lakini pia Moyo unantuma kuwa penzi ni kama Jua, watu wa Arusha wakilalamika kutokuliona kwa siku tatu, watu wa Dsm wao wanalala kwamba Jua limezidi! Kwa mara nyingine najiona katika mtihani wa kujitakia, lakini sipaswi kulaumiwa![/SUB]
[SUB]Wakati naiangalia stand ya basi ya Ubungo kwa mara ya mwisho, huku basi likiingia Morogoro road kwa mwendo wa kuskilizia, kibaridi cha kizushi cha alfajir kinakatika, kijua cha kimbea cha Dsm kinachomoza, nilishaanza kuzoeana na John, raia wa Uganda, ambae hakutumia muda mwingi kufunguka kwangu.
Sijui hata alijiamini nini? Hakunificha kitu, alinieleza kuwa safari yake mwisho ni Johannesburg, anaemfuata ni mshikaji wake tu wanaejuana tangu Kampala, ana namba ya simu ya huyo jamaa yake lakini hajui mtaa wala eneo anakoishi, achilia mbali anakofanya kazi, John hana viza, ana passport tu, hajawahi kusafiri hata mikoa ya ndani ya Uganda! Anasema safari yake ya kwanza ni Kampala Dsm. Kuhusu shule alisema, kusoma ni kipaji, na yeye hakuwa nacho![/SUB]
[SUB]John akataka kujua kuhusu mimi. Na mimi bila kusita nikafunguka. Niliamini kuwa safari kama hizi siwezi kukosa marafiki kama ilivo kuwa siwezi kukosa na maadui! Nikasema huyu ni wa kwanza, kama ni adui ama rafiki, nitamjua baadae![/SUB]
[SUB]Nikamuelezea yote kuhusu Safari yangu.
Na hasa dhamira yangu kuwa naenda Cape town, na huko kuna ndugu, jamaa na marafiki waliojipa uraia wa South, na kwamba nina mawasiliano nao ya karibu wakiwemo watatu nilioongea nao punde tu pale ubungo, kuwafahamisha kuwa nshaanza safari.
Nilimueleza kuwa nimegonga viza ya siku 90 na kwamba niko vizuri kwa safari, na niko tayari kwa lolote litakalojitokeza njiani! Nikamueleza kuwa nimemaliza chuo na kwamba ujana unaniruhusu kupambana na maisha kwa aina yoyote ile vita, hii ni mojawapo tu! [/SUB]
[SUB]Tuliongea mengi sana, ikiwemo mambo ya familia na matarajio huko kwa watu. John alionyesha na kusikitishwa kwa mtu mwenye elimu ya chuo, kukimbia nchi yake, kwake yeye mtu anaepaswa kukimbia nchi ni yule asiye na elimu tu, wenye elimu wabaki kujenga nchi! Ni kama alikuwa anampigia mbuzi gitaa, sikutaka kumuelewa![/SUB]
[SUB]Mazungumzo yangu na John, yalifanyika katika lugha ya Kiswahili. Kumbe pale mbele Milgo na Fatma walikuwa kimya wakijaribu kuskiliza kila kinachozungumzwa kati ya mimi na John, na walifanikiwa kukamata sehemu kubwa ya mazungumzo yetu! Hili lilikuwa jepesi sana kwa vile Milgo alikuwa ana uelewa mkubwa wa Kiswahili huku Fatma akiwa anaibiaibia, walikaa kimya na ukimya wao ulimaanisha kuzidisha umakini katika mazungumzo yangu na John.
Faida ya kwanza ya mimi kufunguka kwa John ikaonekana, ni pale Milgo alipojipa ujasiri na kuingilia mazungumzo yetu, nikaone hii sasa ni bahati ya mtende (kwa faida yako tuu, mizizi ya miti mingi hutambaa kufuata uelekeo wa Maji, Mtende ndio uko tofauti kwa vile wenyewe mizizi yake hufuatwa na maji) na wenye bahati kama hizi tupo wachache sana![/SUB]
[SUB]Ule mnyukano wa Akili na Moyo wangu, nilishausahau kwamba uliishaje. Zile nasaha zote kuhusu kuwa makini safarini, sikumbuki kama niliambiwa mimi, Yule homeboy wangu alienisisitiza sana pale Ubungo eti nikae mbali na warembo, najua ni wivu tu ulikuwa unamsumbua, nilishaachana na shauri zake zile. Hata kipindi hiki ambacho Milgo ameonyesha kuvutiwa na maelezo yangu, John aliejaribu kunisihi nipunguze mazoea na Msichana huyu wala hakufanikiwa, kwangu niliamini kazi na dawa![/SUB]
[SUB]Milgo alikuwa na Maswali mengi sana kwangu kuhusu safari, tena wakati wote wa mazungumzo walionyesha kitu kama kutotambua uwepo wa John, Mganda, kwangu hiyo niliona ni kete, tena muhimu sana kwa kuamua matokeo, kitu kizuri ni kwamba kila jibu nililompa Milgo lilikuwa ni jibu alilopenda kuskia.Kwa kina Milgo ilikuwa ni kama wana bahati kubwa kumjua mtu mwenye malengo kama yao, yaani wote ni wasafiri wa Cape town wakitokea Kenya.
Milgo alivutiwa zaidi na uwezo wa kujiamini, hata nilipomuambia kuwa mimi si mzoefu wa safari za South, hakuamini, alifurahi zaidi alipojua kuwa mimi ni Mtanzania, kwao wao watanzania ni watu wakarimu sana, na hapa amepata fursa ya kuuona ukarimu wa watanzania, lakini la muhimu zaidi ilikuwa ni kujua kuwa katika timu hii ya watu wane, kuna mtu mmoja ana viza, tena mtu huyo ni mtanzania![/SUB]
[SUB]Yaani mpaka tunaingia Al Jazeera, sikumbuki kama basi lilipita Chalinze wala Msamvu pale Morogoro, ninachokumbuka tu ni kwamba sasa tupo Al Jazeera, namna tunavoonekana, inahitaji uwe mbeya aliekubuhu kuuliza kama kuna uhusiano wowote kati ya Milgo na Mimi! Ulichopaswa kufanya wewe ni kupigia mstari tuu! Hakuna cha kuuliza hapa. Jamani safari mbona imekuwa fupi hivi!
[/SUB]
[SUB]Wakati tunashuka kutoka kwenye basi, John alikuwa wa kwanza, akifuatiwa na Fatma, nyuma ya Fatma nilikuwa mie, na mwisho ni Milgo! Katika hali ambayo sikuitegemea, Milgo alinivuta mkono ghafla, nilipogeuka na kutaka kumuuliza kuna nini akawahi kuuweka mkono wake mdomoni mwangu kufanya sauti isitoke! Kisha akanivuta kuelekea pembeni, ni kama vile kaona kitu tofauti na anataka kunambia, afu ghafla![/SUB]
Cc ram loveissweet baby v

Last edited by a moderator: