Abdallah Masoudi
Member
- May 6, 2019
- 9
- 4
MPENZI:
Mpenzi laazizi nyonga mkalia penzi,
Nakupenda kama njaa ipendavyo shibe,
Nimeamua hili huba kulitilia tui la nazi,
Nitaliundia na kamati ya ulinzi wasiliibe.
Unajua nini babe, sio tu nakupenda la hasha!
Napenda kujiona navyokupenda wewe,
Wakisema nakupenda pia nabisha,
Naweza sema ni zaidi ya kukupenda maana nipo radhi kuzikwa nawe.
Ungekuwa pombe basi ningelewa chakari,
Ungekuwa ngumi mimi ningekuwa Mandonga,
Ungekuwa chai kwangu ningekuwa sukari,
Ungekuwa chawa nami ningekuwa kitonga.
Nakupenda mpaka napenda kujiona navyokupenda,
Nakupenda hadi upendo unatamani niwe mpenzi wake,
Kwa hatua tuliofikia nahisi mimi Pete nawe chanda,
Nikiwa nawe natamani nikukumbate au nikurushe rushe juu nikudake.
Mpenzi umetunukiwa mahaba,
Wewe ni tunu mtoto wa mama mkwe,
Njoo tucheze kibaba baba,
Anazeeka yule tumpelekee mjukuu wake.
Nanadi sifa zako huku naringa mpenzi,
Yani kama nguo zinavyonadiwa na Chinga,
Unajua kwako fika sijiwezi,
Moyo wangu nimekupa wewe chunga.
0674855951