Ufipa-Kinondoni
JF-Expert Member
- Jan 3, 2012
- 4,582
- 2,783
MBOWE ANATAKIWA AJIUZURU SIYO KUPENDEZEKEZA KATIBU MKUU WA CHADEMA.
Kwa maoni yangu kutokana na mwenendo wa siasa ndani ya Chadema, na kutokana na matokeo ya uongozi wa Mwenyekiti wa Chadema ndugu Freeman Mbowe, kwenye kikao cha Baraza Kuu kesho Mbowe anatakiwa ajiuzuru na siyo kupendekeza jina la Katibu Mkuu wa Chadema. Ninazo sababu za kuunga mkono mtazamo wangu.
1. Chadema imeshindwa kushinda uchaguzi mkuu uliopita chini ya uongozi wake. Uongozi wake uliweka mikakati kadhaa ya kushinda uchaguzi ikiwemo kumleta Lowassa. Mkakati huu umechangia kwa asilimia nyingi kupoteza ushindi. Lowassa ilikuwa ngumu kumuuza. Watanzania walimkataa. Aidha utaratibu wa kumwondoa Dk Slaa ulikuwa wa mizengwe pia ulichangia kukikosesha chadema kura. Demokrasia haikutumika kumtoa Dk Slaa na kumleta Lowassa. Yalitumika mabavu. Gia ilibadilishwa angani.
2. Uteuzi wa wabunge wa viti maalum, ni suala ambalo limegubikwa na masuali mengi na ya aibu. Haya yote yamefanyika chini ya uongozi wake. Mbowe akae kando hasitahili kumteua Katibu Mkuu.
3. Wakati wa Kampeni 2015, uongozi wa chama haukuweza kuwasaidia wagombea kwenye maeneo yote isipokuwa baadhi tu ambako yeye na kikundi chake walikuwa na maslahi. Haiwezekeni mikoa iliyoongoza kwa uamsho kama Shinyanga, Mwanza, Simiyu, Geita na Tabora ikose mbunge hata mmoja. Nguvu nyingi za chama hazikupelekwa huko.
3. Chadema haina ajenda kwa sasa hasa juu ya kupinga ufisadi na rushwa. Wakati wa kura za maoni wananchi walishuhudia rudhwa ndani ya Chadema kuliko hata ccm mpaka wananchi wakaikataa chadema. Mbowe jiuzuru, hustahili
Kupendekeza Katibu Mkuu wa Chadema.
Hayo ni maoni yangu.
Fred Mpendazoe.