Mpasuko CCM Arusha

Huyu ameshushwa timu b akisha pasha misuli atarudishwa timu a kwani alichelewa kuripoti akamkoromea bosi wa timu ndio kaamua kumpa adhabu hiyo kwahiyo atarudi timu a muda si mrefu.
 

Mkuu naomba nikusahihishe, victor ambaye ni mgombea wa CCM anatokea tawi la corridor area na sio fire, pia hapo fire hakuna anayetaka kusikia habari ya ccm kabisa na Ndarivoi huwa anapata kura 3 eneo hili.
Kaburu wa chadema anaishi tawi la themi mashariki(njiro) na anaungwa mkono na wapiga kura wa matawi yote manne likiwemo la fire.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Arusha msituangushe lazima ukombozi uanzie huko! Up CDM, up M4C
 
CCM na CUF ni kama vile mama mmoja baba mbali mbali
 
Ameenda chama muafaka maana chadema haitaki watu wanataka madaraka tu tunataka cc watu makini na wenye moyo wa kuleta maendeleo. safi sana ametoka A na kuingia B
 
Arusha msituangushe lazima ukombozi uanzie huko! Up CDM, up M4C

Mkuu hatutawaangusha,
Tumejipanga CHADEMA tunachukua kata zote 4 easily kama kupapasa maiti.

M4C with no apology.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 

Paradiso!
Asante kwa taarifa ila HAPANA/NO KABISA CHADEMA haitumii njia ya eti 'vita ya panzi' Kitu kinafanyika ni elimu kwa umma na umma unaamua kubagua mchele na changarawe.
Pia kumbuka CUF ni tawi la CCM kwa hiyo hapo wanacheza kete ya kugawa kura za CHADEMA
 
jaaamani huyu Ndaravoi ni jirani yangu kabisa pale themi. namjua jinsi alivyomjinga! elimu yake kubwa ni darasa la 7, na alivyoshinda kura za maoni ccm, aliwatukana sana wagombea wenzake wa ccm, na alisema amewabwaga wasomi wote!
 
Kitendo cha baadhi ya pro chadema kukikashifu chama cha CUF si cha kingwana hata kidogo,kama kukiita CCM B,au MKE WA CCM n.k,lazima watu watambue ya kwamba CUF pia ina wafuasi wengi tanzania,ifikie wakati kuwa na uvumilivu baina au miongoni mwa hivi vyama vya upinzani,kama wote nia ni moja kuiondoa CCM madarakani haionekan kwa kuwachukia CUF waz waz ni kuwapa CCM ushindii??

Mitanzania mingine hopless sana,wakenya wana mengi ya kuwafunza lakini watu wanajotoa ufaham bure bure...
 
Hizi kata nne tayari zishachukuliwa wapende wasipende, mi ninachotaka kujua kata ya Sombetini imekwamia wapi?
Kwanini isitangazwe kuwa iko wazi wakati haina diwani?

Mimi nafikiri kamanda mawazo arudi kwenye kata atangaze yeye ni diwani,lakini kupitia CDM halafu tusikie watasema
nini kuwa kata haina mtu au watakubali kuwa bado ina diwani'
 
cuf kumbe ina wafuasi na si wanachama, kama lengo la upinzani ni moja, mbona bungeni wanaosikika ni wabunge wa chadema na nccr mageuzi tu? Hawa wa cuf wamebaki kuisemea zanzibar tu, labda magdalena sakaya!
 

Hajahama Nyumba amehama chumba huyo.
 
Mkuu kura zinazogawanywa hapa ni za ccm.
Huyu kada wa ccm aliyeamia cuf amesababisha mpasuko ndani ya ccm ivyo ni wazi ameamua kugombea kupitia cuf kwa maksudi ili kupunguza kura za ccm kwasababu anajua hawezi kushinda.
Yani ameamua kufanya mchezo wa 'tukose wote'

Chadema inashinda kata hizi 4 za arusha kwa uzembe wa ccm na msuguano wa kambi za ndani ya ccm,
Kikubwa zaidi ni elimu ya uraiya imewaingia wapiga kura kupitia m4c.


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…