Mpango wa Magufuli na CCM kwenye mambo ya afya

Mpango wa Magufuli na CCM kwenye mambo ya afya

Dr.Mo

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2012
Posts
3,809
Reaction score
1,653
Nimemuangalia Magufuli akiongelea kuhusu masuala ya afya na kutoa ahadi mpya nyingi, mimi kama mdau wa afya ntaongelea kidogo hili jambo.
-Kwanza Magufuli na viongozi wengi hasa wa CCM, wanaonekana maswala ya afya na matatizo yake hawayajui kwa undani, na huongea mambo ambayo kwa kweli huyasikia juju na mitaani. Kwa mfano anaposema MADAKTARI na MANESI wanaiba dawa hospitali na kupeleka pharmacy zao nje ya hospitali sio kweli kwa sababu mbili.
1.Hizo pharmacy nje ya hospitali nyingi si za wafanyakazi wa afya, nyingi ni za matajiri wa kawaida hasa MAKADA wa CCM na ndo maana utaona hizo pharmacy zipo miaka nenda rudi, hakuna aliyezifunga, kuzichukulia hatua kwa kununua dawa za magendo kutoka hospitali au takukuru kukamata daktari au nurse yeyote kwa kuuza dawa pale.

2.Hospiitali nyingi za serekali hakuna dawa, mimi kuna kipindi nimefanya kazi hospitali hapo Dar, hakuna dawa labda viantibiotics kama ampicillin na paracentamol lakini huwezi kuta dawa za pressure, sukari, antibiotics kubwa kubwa. na hata kama zipo ni kwa siku mbili tatu zimeisha, sasa hizo dawa za kuiba zinatoka wapi..!? Kuna kipindi tulikua wodi ya akina mama(labour) inabidi wakati mwingine madaktari na murse mjichange kuninua CANULA ya kumwekea mama aliyejifungua maji, au kununua dawa kama oxytoc kwa ajili ya kusidia kinamama hasa wakati wa emergeny.
Kuna watu wanamshangilia magufuli lakini nani hajui kama una mama mjamzito inabidi anunue kit ya kujifungua na kwenda nayo hospitali..!?

-Ukija kwenye matatizo ya vitanda hospitali limekuwa tatizo sugu kama lilivyo la madawati shuleni...huwa najiuluza ivi serekali na CCM wangeamua hili tatizo lisinge isha una magereza na jkt wanatengeneza mpaka gari(nyumbu) wanashidwa kutengeneza vitanda kwa ajili ya hospitali..? Au ni utashi wa kuamua hakuna na ccm wanaona hawa MALOFA na WAPUMBAVU watalala chini tu.

-Ukiangalia kwa miaka ambayo KiKwete na CCM wamekuwa madarakani, wamepunguza kusponser wanafunzi kwa ajili ya masters mbali mbali, imepelekea kupunguza uzalishaji wa madaktari bigwa kupeleka hasa mikoani na wilayani(wakati huo wanaita hospitali za mikoa za rufaa) hapitali inakuwaje ya rufaa bila specialist na vifaa na dawa..

Leo Magufuli anasimama jukwani anaimba ngonjera na watanzania wanamshangili na kusema anasera..magufuli atafanya nini zaidi CCM wameshidwa kufanya good 50 years. Kweli mkapa hakukosea WABONGO ni MALOFA na WAPUMBAVU.
Hila la afya na elimu CCM wasidanganye watu, Miaka yote hawakuwa na nia ya kutatu matatizo kwa dhati. Magufuli ni vuvuzela..
 
Msd mpaka iligoma kutoa dawa kutakana na deni kubwa la zaidi Ya 90Bilion.
Sasa hivi bank hazina damu kwa sababu msd serikali hajatoa pesa za kukukusanyia damu na vitenganishi vya kupimia damu iwe salama nayo hii madaktar wa nakunywa damu hadi bank hazina damu.
Magufuri hujui aliongealo kwa malofa
 
Ndo mambo ya kujiuliza hayo kama huwezi kupima Damu kuhakikisha ipo salama, sijui inakuwaje unashidwa hata kueleawa, kama msd inaidai serekali bilioni 90 unategemea wanafanyaje kazi..!

Hili la kuiba dawa na kuuza pharmacy nje sijui kwa nini watu wanalishabikia kwanza dawa za serekali(msd) zinakuwa na lebo(nembo), alafu kwa nini wasikamate hasa takukuru au tungesikia pharmacy moja imefungiwa kwa sababu ya kununua dawa kutoka serekalini..ccm waache usanii..?! Ila hawawezi kuacha kwasababu wanajua watanzania ni MALOFA na WAPUMBAVU..na bahati mbaya UKAWa wmelala huku bao la mkono likitengenezwa machoni mwao..
 
1. Hawezi kuleta sera za kukamata daktari/muuguzi mwenye duka lake la dawa. Mishahara yenye makato makubwa huyu mtumishi akajipatie wapi kwa taaluma yake?

2.Hali ya hospitali nchini ni mbaya, bohari ya madawa nayo iko hoi, hivi kweli dawa hospitali nchi nzima zinaweza kuibiwa? Mbona ni kuukana taaluma za watu kuwa ni wezi? Halafu ukiwatusi namna hii unatwgemea nini toka kwao iwapo waliwahi kudai(madai yao wakaambiwa ni kudai fedha tu)?
-Dawa za MSD si zina chapa/label?
-Kama ni kweli wapo wale wanaoiba kwanini wasikamatwe(hili si ni ombwe kiuongozi)?
Okay(hypotheticaly speaking wanaiba dawa), hivi na vitanda navyo wanaiba? Damu wanakunywa? Vifaa tiba wanapeleka katika maduka yao?

3.. Ufadhili wa masomo ulioungelea hapo ndiyo mbaya zaidi. Mwaka jana Wizara ya Afya ilitoa ufadhili kwa wanafunzi 100(mia moja tu) wa taaluma mbalimbali za Afya na ikatoa msimamo kuwa hii itaendelea kupungua. Mwaka huu wanafunzi waliochagulia kujiunga na vyuo kwa kozi mbalimbali za shahada ya pili(Masters) nia ya tatu(Superspecialization) ni zaidi ya 700(na hapa kukiwa na vyuo vinavyoendelea kupokea maombi mf. Muhimbili inaendelea kupokea maombi hadi kesho tarehe 28)

-Wataalamu wa Afya walikuwa wakimaliza masomo yao(kuhitimu) WANAFANYA KAZI chini ya usimamizi (Hii ni duniani kote, na baadhi ya taaluma hili si jambo geni), wiki mbili zilizopita wizara imetoa fomu maalum kwa wahitimu mbalimbali(udaktari, ufamasia n.k) kujazwa kwa wale waliomaliza mwaka huu KUKUBALI kuwa watafanya kazi kwa miezi kumi na mbili POPOTE watakaoopangiwa na Serikali bila malipo.

Then unajiuliza, hivi dunia hii ya ushindani unategemea utamlazimisha mtu haya huku nchi jirani kuna uhitaji(ingawa si mkubwa kana kwetu lakini malipo yao ni mazuri)?

Ni nani atakubali mwanae/ndugu mzaliwa wa Tanga/Kagera n.k aende Sumbawanga, Songea, Geita, Dar kukaa mwaka mzima bila malipo?
Hivi hawa wakianza kupokea "ahsante" tena ile ya kabla ya huduma, mtawalaumu?
Wakiamua kufanya kazi kwa jinsi wanavyotaka mtawashangaa?
Wakiamua kuiba dawa kweli kweli, hamtawaelewa?

Watanzania tunapenda mambo rahisi, na wakati fulani tunapenda kusikia vitu vizuri(kusafisha masikio na mioyo yetu) kwa sabanu ya shida zilizotujaa. Tumekuwa waoga kufanya mabadiliko.

Leo hii mifuko midigo midogo ya Bima imefutwa(hata kule kijijini) Community Health Fund, (CHF) wafanyakazi/watumishi wenye BIMA bado wananyanyaswa hospitali nyingine, na wengine hununua dawa desoite kukatwa kila mwezi kwasababu tu BIMA haikubaki dawa hizo. Leo vioja vile vile vinarudiwa! Vikisemwa na madktari na watumishi wa afya(ni shida kwani wao wanataka hela tu), vikisemwa na wagombea hilo ni sawa na linaweza kutekelezeka.

Sawa ngoja tuendelee kufurahisha masikio na mioyo yetu.
 
Matajiri waliokuwa wanaisumbua ccm, wamehama au watahama na Lowasa, Magufuli ana nafasi kubwa ya kuunda serikali bora na yenye ufanisi kuliko lowasa, ambaye kiubinadamu atalazimika kulipa fadhira kwa marafiki zake walikuwa wanamchangia pesa za kampeni. Funguka mtanzania, dk Slaa kukimbilia mafichoni so mjinga.
 
Nimemuangalia Magufuli akiongelea kuhusu masuala ya afya na kutoa ahadi mpya nyingi, mimi kama mdau wa afya ntaongelea kidogo hili jambo.
-Kwanza Magufuli na viongozi wengi hasa wa CCM, wanaonekana maswala ya afya na matatizo yake hawayajui kwa undani, na huongea mambo ambayo kwa kweli huyasikia juju na mitaani. Kwa mfano anaposema MADAKTARI na MANESI wanaiba dawa hospitali na kupeleka pharmacy zao nje ya hospitali sio kweli kwa sababu mbili.
1.Hizo pharmacy nje ya hospitali nyingi si za wafanyakazi wa afya, nyingi ni za matajiri wa kawaida hasa MAKADA wa CCM na ndo maana utaona hizo pharmacy zipo miaka nenda rudi, hakuna aliyezifunga, kuzichukulia hatua kwa kununua dawa za magendo kutoka hospitali au takukuru kukamata daktari au nurse yeyote kwa kuuza dawa pale.

2.Hospiitali nyingi za serekali hakuna dawa, mimi kuna kipindi nimefanya kazi hospitali hapo Dar, hakuna dawa labda viantibiotics kama ampicillin na paracentamol lakini huwezi kuta dawa za pressure, sukari, antibiotics kubwa kubwa. na hata kama zipo ni kwa siku mbili tatu zimeisha, sasa hizo dawa za kuiba zinatoka wapi..!? Kuna kipindi tulikua wodi ya akina mama(labour) inabidi wakati mwingine madaktari na murse mjichange kuninua CANULA ya kumwekea mama aliyejifungua maji, au kununua dawa kama oxytoc kwa ajili ya kusidia kinamama hasa wakati wa emergeny.
Kuna watu wanamshangilia magufuli lakini nani hajui kama una mama mjamzito inabidi anunue kit ya kujifungua na kwenda nayo hospitali..!?

-Ukija kwenye matatizo ya vitanda hospitali limekuwa tatizo sugu kama lilivyo la madawati shuleni...huwa najiuluza ivi serekali na CCM wangeamua hili tatizo lisinge isha una magereza na jkt wanatengeneza mpaka gari(nyumbu) wanashidwa kutengeneza vitanda kwa ajili ya hospitali..? Au ni utashi wa kuamua hakuna na ccm wanaona hawa MALOFA na WAPUMBAVU watalala chini tu.

-Ukiangalia kwa miaka ambayo KiKwete na CCM wamekuwa madarakani, wamepunguza kusponser wanafunzi kwa ajili ya masters mbali mbali, imepelekea kupunguza uzalishaji wa madaktari bigwa kupeleka hasa mikoani na wilayani(wakati huo wanaita hospitali za mikoa za rufaa) hapitali inakuwaje ya rufaa bila specialist na vifaa na dawa..

Leo Magufuli anasimama jukwani anaimba ngonjera na watanzania wanamshangili na kusema anasera..magufuli atafanya nini zaidi CCM wameshidwa kufanya good 50 years. Kweli mkapa hakukosea WABONGO ni MALOFA na WAPUMBAVU.
Hila la afya na elimu CCM wasidanganye watu, Miaka yote hawakuwa na nia ya kutatu matatizo kwa dhati. Magufuli ni vuvuzela..

kwani wewe ni raia wa nchi gani embu soma hii Ilani vizuri kwanza katika suala la AFYA

· kwa Afya: Kuhakisha kwamba kila kijiji kinakuwa na Zahanati, kila Kata inakuwa na Kituo cha Afya, kila wilaya inakuwa na Hospitali, na kila Mkoa unakuwa na hospitali ya Rufaa:
· kuwapatia mafunzo watumishi wake ndani na nje ya nchi; kwa

· kuzipatia vifaa bora na vya kisasa hospitali zetu kama vile mashine za mionzi (LINAC machine) kwa ajili ya tiba ya saratani; kununua mashine za mionzi kama vile CT-Scan na MRI kwa ajili ya upasuaji wa ubongo na mgongo.

· Lengo la kufanya hivyo ni kuwezesha upatikanaji wa huduma mahsusi zinazohitaji vifaa na ujuzi mahsusi zipatikane hapa hapa nchini na hivyo kutolazimika kupeleka watu wetu kutibiwa nchi za nje. Aidha, kuajiri wataalamu zaidi wa afya kutoka ndani na nje ya nchi pamoja na kuboresha mazingira ya kazi kwa lengo la kuongeza ubora wa huduma za afya. Hospitali za Wilaya zitaendelea kuimarishwa kwa kuzipatia madaktari, wauguzi, dawa na vifaa tiba vya kutosha. Pia tutatoa motisha kwa watumishi ambao wanafanya kazi katika maeneo yenye mazingira magumu ili kuwajengea ushawishi wa kuendelea kutoa huduma za afya katika maeneo hayo. Utaratibu pia utawekwa utakaowezesha wananchi kuwa na Bima ya Afya ili kumudu gharama za matibabu.
 
Matajiri waliokuwa wanaisumbua ccm, wamehama au watahama na Lowasa, Magufuli ana nafasi kubwa ya kuunda serikali bora na yenye ufanisi kuliko lowasa, ambaye kiubinadamu atalazimika kulipa fadhira kwa marafiki zake walikuwa wanamchangia pesa za kampeni. Funguka mtanzania, dk Slaa kukimbilia mafichoni so mjinga.
Usikimbie ngoja nkuulize maswali..
1.Ntajie matajiri watano wanaomchangia hela lowasa.
2.Ntajie matajiri watano waliohama na lowasa au watakao hama na lOwasa..!?
 
kwani wewe ni raia wa nchi gani embu soma hii Ilani vizu
Ilani ipi, kwani miaka yote ccm ambayo kuna matatizo ambayo yanatatuliwa kwa akili ya kawaida kulikuwa hamna ilani, au ya sasa hivi imeandikwa kwa dhahabu...!? Mna bahati sana NEC itawabeba
 
Matajiri waliokuwa wanaisumbua ccm, wamehama au watahama na Lowasa, Magufuli ana nafasi kubwa ya kuunda serikali bora na yenye ufanisi kuliko lowasa, ambaye kiubinadamu atalazimika kulipa fadhira kwa marafiki zake walikuwa wanamchangia pesa za kampeni. Funguka mtanzania, dk Slaa kukimbilia mafichoni so mjinga.

Nonsense and Out of the topic, hii si kampeni tunajadili ukweli. Afya ya mtu haina uchama, kumbuka hilo. Hata madaktari(pamoja na kuwa na vyama vyao wether CCM,TLP, TADEA etc) wangekuwa wanakuuliza chama chako au upenzi wa chama gani kabla ya kutoa huduma tusingefika. Tusilete ushabiki katika hili.

Anyway, kwani shida hizi zimeanza wakati huu wa kampeni? JK hazijui? At his very best words "sitawaangusha nitayaendeleza yaliyofanywa na Mzee Kikwete"

Seriously, hata kutoa chanjo tu kwa wafanyakazi(waliokatika mazingira hatarishi) hamwezi then mnasema nini?

Afya ibaki kuwa Afya siasa zibaki kuwa siasa.
 
Tuliokuwa kwenye kada ya Afya tunajua hali halisi. Malofa tunadanganywa jamani
 
Back
Top Bottom