Ngoja nivunje ukimya kwenye hii thread. Mkuu supporters wa upizani (na labda vyama vya upinzani vyenyewe) haswa mwaka huu wana nishangaza sana. They are so confident kwamba wata shinda lakini at the same time wamesha andaa defense mechanism ya kwamba wata zulumiwa. In short kwao uchaguzi kuwa huru na haki ni wao tu kushindwa ila wakishindwa basi wame fanyiwa foul.
Mkuu kama upinzani ikishinda ita kuwa very obvious na wala CCM hawata weza kuficha. Kwa mfano nasikia apparently polls nyingi zina mpa Dr. Slaa around 65-75%. Tanzania mtu kushinda uraisi ana hitaji 50%+1 kushinda. Sasa kama Dr. Slaa ana pewa chance kubwa hivyo ya kushinda assuming ana pata kura idadi hiyo CCM wata ziibaje na kuzi punguza mpaka ziwe chini ya 50%+1?
Kuna mtu mmoja alisha wahi kusemaga "In Africa elections are only free and fair when the opposition wins". Hii ni demokrasia mkuu. Msi tangaze ushindi wa kishindo lakini at the same time mna kimbilia kusema kura zitaibiwa. Wengine wana jiuliza kama nchi ita kalika CCM ikishindwa mimi najiuliza kama hali ita kuwa tulivu kama upinzani ukishinda.
Well nime fungua mkuu na kwa ufunguzi huu I guarantee thread yako ita pata replies nyingi. Na mimi ngoja nijitetee mapema nisema nasubiria kukaangwa na mashabiki wa raisi mteule Dr. W. Slaa.