Mpanda: Watatu wafariki dunia wakisafirisha magendo

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,717
55,819
Katavi.

Watu wa tatu ambao ni wakimbizi kutoka Nchi ya Burundi wanaoishi katika makazi ya wakimbizi ya Katumba mkoani Katavi wamekufa papo hapo bada ya gari waliliokuwa wamepanda wakiwa wanasafirisha magogo kuacha njia na kisha kupinduka.
18447076_1367083956707813_4881443665617282485_n.jpg

Ajari iliyosababisha vifo vya watu hao ilitokea Mei 8, majira ya saa 9;30 usiku katika Kijiji cha Kanoge, Makazi ya wakimbizi ya Katumba Wilayani Mpanda ambapo watu hao walikuwa wakisafirisha kwa magendo magogo ya mti wa mkurungu ambao ni kosa kisheria kukata miti hiyo.

Akitoa taarifa ya tukio hilo Kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi Damas Nyanda alisema kuwa ajali hiyo ililihusisha gari lenye namba za usajiri T 880 BNX aina ya Mitsubish lililokuwa likiendeshwa na dreva aliyejulikana kwa jina moja la Boni ambae ndie mmiliki wa gari hilo.

Alisema gari hilo lilikuwa likitokea Katumba katika makazi ya wakimbizi likielekea mjini Mpanda na lilikuwa limepakia magogo hayo ya Mkurungu ambayo walikuwa wakiyasafirisha kwa magendo nyakati hizo za usiku.

Waliokufa katika ajali hiyo majina yao hayaja julikana bado lakini ni wakimbizi wanao ihi katika makazi hayo na mili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Hositali ya Manispaa ya Mpanda kwa ajiri ya kutambuliwa na ndugu zao.

Kamanda Nyanda alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kutokana na mwendo kasi wa dereva wa gari hilo hali iliyosababisha dereva wa gari hilo kushindwa kuliumudu na kugonga gema pembeni ya bara bara na kisha kupinduka.

Alisema Dreva wa gari hilo alikimbia mara baada ya kutokea kwa ajari hiyo na jeshi la Polisi linaendelea na msako wa kumtafuta ili aweze kujibu mashitaka yanayomkabili.

Kamanda huyo wa polisi ametoa wito kwa madereva kufuata sheria za usalama barabarani na wamiliki wa magari waache tabia ya kusafirisha bidhaa ambazo ni zamagendo kwani ni hatari kwa usalama wao na vyombo vya moto wanavyo endesha.
 
Back
Top Bottom