Elections 2010 Mpambanaji wa ufisadi james lembeli wa ccm imekula kwake???

minda

JF-Expert Member
Oct 2, 2009
1,068
65
kwenye uchambuzi wa magazeti wa radio mbalimbali leo tumepata kusikia ya kwamba mkurugenzi wa uchaguzi rajabu kiravu amekanusha uwepo wa jimbo jipya la ushetu.

siku za karibuni imepata kusemwa ya kwamba lembeli alilikimbia jimbo la kahama na kuchukua fomu kwenye jimbo jipya la ushetu.

Lembeli amekuwa katika mvutano mkali wa kisiasa, kati yake na viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayani Kahama.

Uamuzi wa mbunge huyo kuhamia katika jimbo jipya, uliutangaza juzi baada ya Katibu wa CCM wa Wilaya ya Kahama, Sospeter Nyigoti, kutangaza kuwa wamepokea taarifa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kuwa imekubali kutangaza Jimbo ya Ushetu.

Baada ya taarifa hiyo, Lembeli alichukua na kujaza fomu ya kumwezesha kuomba kuteuliwa ili awanie ubunge katika jimbo hilo jipya badala ya jimbo lake la awali.
gonga hapa

sasa kwa mtindo huu sio kwamba lembeli sasa amekufa kisiasa? na huenda sio adhabu kwa kukosa staha? au tuseme chama chake kimeamua kumuingiza chaka ili apotee kwenye tasnia ya siasa hasa ikizingatiwa kuwa alikuwa katika mvutano na uongozi wa chama chake wilayani?

yeyote mwenye thread atujuze ili tuwe na uhakika na ishu hii.
 
mbinu chafu zitasababisha watu wauane tena kikatili kama mambo yenyewe ndiyo haya!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!tayari wengine wameshakamatwa na miguu ya binadamu cjui kama sio ya albino.....
 
ha hha ha nacheka kwa kuona watu wanavyotumia mbinu zisizo fikirika .bila shaka wamemfanyia mchezo mchafu waalijua fika kuwa hilo jimbo halipo hivi inawezekanaje katibu wa chama {TAWALA} wa wilaya atoe fomu kwa mtu kwa kutegemea tetesi , sasa hapo kurudi kahama hawezi na jimbo ushetu {tetesi} halipo wamemuacha njia panda
 
Huyo Lembeli naye ni wa ajabu? Anaishi karne ya wapi ashindwe kuelewa ulaghai huo? Hii ni kali sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom