Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,614
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu ya SMZ ndugu Charles Hillary ametoa tangazo kwa umma ambalo clip yake inatrend kwamba eneo la shamba la Makurunge Razaba lililopo Wilaya ya Bagamoyo Kata ya Makurunge lenye ukubwa wa hekta 6000 ni mali ya SMZ tangu 1977. Haruhusiwi mtu, kikundi au taasisi kufanya shughuli yoyote katika eneo hilo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu au kikundi cha watu kitakachokwenda kinyume na tangazo hilo, aidha serikali haitakuwa na wajibu wa kulipa fidia kwa mtu yeyote aliyepatiwa eneo katika shamba hilo.
Maswali-fikirishi:-
1. Mpaka wa Znz na Tanganyika uko Bagamoyo au baharini?
2. Ardhi ya Tanganyika inamilikiwa na Marais 2 wa SMZ na Muungano?
3. Je, ardhi ni rasilimali/sekta/wizara ya muungano?
4. Serikali imetangaza kwenye Bunge linaloendelea kwamba imepunguza kero za muungano je, hii ni kero mpya imetengenezwa?
5. SMZ ikisema hilo eneo ni lao na serikali ya muungano ikaridhia je, SMZ haitawauzia Waarabu kama wanavyouza visiwa vile 52?
6. Je, namba 5 hapo juu ikitimia TRA itakuwa na mamlaka ya kukusanya mapato toka kwa hao Waarabu? Au ni ZRA ndiyo itakusanya mapato hapo?
7. Hizo namba 5 na 6 zikitimia je, TRA na ZRA zitalazimika kuchora ramani upya ya nchi kuona wigo wao kijiografia unaanzia na kuishia wapi?
8. Je, Bunge hili haliwezi kujadili suala hili?
9. SMZ ikimiliki ardhi hiyo Tanganyika, vipi siku moja inaweza kulifanya jimbo lake la uchaguzi? Eneo hilo kwa saizi za majimbo ya Znz linaweza kutoa majimbo hata 10.
10. Hiyo namba 9 ikitimia je, jimbo la Bagamoyo itabidi lifumuliwe na kusukwa upya?
11. Je, SMZ ikiwapa Waarabu eneo hilo alafu JMT nayo ikawapa Wachina sehemu ya Bagamoyo kujenga bandari kubwa Afrika hatima ya Bagamoyo itakuwaje?
12. Nadhani viongozi wetu wajitafakari upya na kujisahihisha kwa mustakabali mwema wa nchi.
13. Balozi Karume amejipa uanaharakati wa kutetea ardhi (visiwa) ya Znz isiuziwe Waarabu, sitaki kuamini kwamba anajitengenezea agenda ya uchaguzi bali nataka kuamini kwamba anatuamsha usingizini Wabara kwa kuanzia na Bagamoyo.
14. Kwanini milki ya eneo hili inasisitizwa kwy awamu ya 6?
15. Hivi Korea Kusini inaweza kuchukua ardhi ya Korea Kaskazini kwa kigezo kuwa wameungana kwenye jina lao la Korea?
16. Je, kumbe tulitakiwa kumuachia Idd Amin Kagera na Mwanza? Huenda leo tungekuwa tunamiliki mafuta ya Ohima kupitia muungano huo?
17. Kumbe Malawi nayo tungeiachia mpaka wa mto Songwe unaohamisha mpaka huo kila masika. Pia kumbe tungeiachia Malawi ziwa Nyasa 100%.
18. Eneo la Makurunge Razaba 6000 ha ni asilimia 2.4 ya ukubwa wa Zanzibar wa 246100 ha (I have used Back-of-the-envelop calculation for implied meaning not explicitly stated)
19. Wamasai wa Kenya walinyang'anywa na kufukuzwa kwenye ardhi yao Ngorongoro (wakati muungano wao ni umasai wao) kwanini na wao wasingeachiwa kama Wazanzibar wanavyoachiwa Makurunge Razaba? Kijadi ardhi ya Wamasai bila kujali mipaka ya nchi ni Ngorongoro, Loliondo, Tarangire, Lake Manyara, Serengeti, Monduli. Ardhi ya Wamasai ni 2.8% ya ukubwa wa JMT. (I have used Back-of-the-envelop calculation for implied meaning not explicitly stated)
20. Nyerere na Karume kuchanganya dongo za Zanzibar na Tanganyika kama ishara ya muungano hakukumaanisha ni nchi moja na kwamba mipaka isiheshimiwe.
21. Kuna utata mbeleni ambao serikali haujauona. Ni hivi, kama SMZ ni mpangaji tu wa eneo hilo (siyo mmiliki) na sheria ya Tanganyika (ardhi siyo rasilimali ya muungano) inasema mpangaji wa ardhi ana haki na vilivyopo juu yake tu (siyo vilivyoko chini) vipi kama mbeleni huko tuendako kukagundulika kuwa eneo hilo lina madini au vito adimu duniani? Si tutakuwa tumetengeneza vita ya wenyewe kwa wenyewe?
22. Kama Zanzibar wana haki na eneo hilo kwamba wao ni sehemu ya muungano, vipi walipiga kelele kuhusu tetesi tuu za mafuta kuwepo kwenye bahari yao kwamba rasilimali-hiyo-dhaniwa siyo ya muungano, kwahiyo wanatufundisha jambo hapa kuwa mali za Tanganyika ni za muungano lakini mali za Zanzibar ni za Zanzibar.
23. Wamalawi wanataka Ziwa Nyasa, Wazanzibar wanataka Bagamoyo, Wakenya wanataka Ngorongoro na mlima Kilimanjaro, Waganda walitaka Kagera na Mwanza, WANA NINI NASI TANGANYIKA!? Tujitafakari upya, yawezekana kuna vitu wanaviona kwetu ambavyo sisi hatuvioni.
Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app