Christopher Wallace
JF-Expert Member
- Dec 8, 2015
- 1,410
- 3,548
Nathubutu kusema sijaona tofauti ya serikali ya JK na JPM wote kwa pamoja walianza majukumu yao ya Urais kwa kasi kubwa huku wakibeba matumaini lukuki toka kwa wananchi wao.
Nani asiyekumbuka semina elekezi ya JK kwa viongozi wake pale Ngurdoto? Nani asiyekumbuka ziara za kushtukiza kwenye sehemu mbalimbali za kijamii kama pale Sokoni Tandale na kutembelea magereza ya Dar (Keko, Ukonga na Segerea) kwa mbwembwe zote miaka 10 iliyopita? Miaka ilienda, JK aliyekuwa chaguo la mungu kwa wananchi wake akapoteza mvuto toka kwa wale waliompenda.
Na sasa maigizo yale yamehamia kwenye serikali ya Magufuli, maigizo ya kutosha kila kukicha toka kwa mawaziri, wakuu wa mikoa na hata wakuu wa wilaya. Magufuli kila kona anatumbua majipu bila kumaliza viini vya majipu, na sasa nae ameingia njia aliyopita JK. Watu wanasimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi kuhusu matumizi mabaya ya ofisi za umma lakini hatupati feedback juu ya hukumu zao. Iko wapi hukumu ya Bade? Edward Hosea na wengineo? Iko wapi ile mahakama ya mafisadi iliyoimbwa kutwa kucha kwenye kampeni? Hayo ni machache.
Nadiriki kusema Bado sijaona tofauti ya Jk na JPM kiutendaji, wewe ambaye umeona nipe mifano ili unishawishi. Wasiwasi wangu baada ya miaka 10, uongozi wa JK unaweza Kuonekana ulikuwa mzuri kuliko wa JPM.