Moyo wangu unavuja damu

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,118
Kutoka tweeter Anaadika mapunda og

Ndugu zangu twitani, poleni na majukumu yenu. Naitwa Gustaph Stephano Mapunda Ni mwalimu na mjasiriamali (Nina miaka 27). Naomba tiririka na uzi huu uone historia yangu na kilichonikuta leo. Unaweza ukanisaidia mawazo nikatoka hapa

Nilizaliwa wilayani Mbinga-Ruvuma mwaka 1993. Sikufanikiwa kupata mapenzi ya wazazi baada ya wao kufa kwenye ajali mwaka 2000. Nilisomeshwa na kulelewa na kaka yangu aliyezaliwa mwaka 1990 (tulipishana miaka 3 tu)
Huyu aliyevaa taifa. Usomaji wangu katika level zote za sec sikuwa kwenye mfumo rasmi. Kwani mwl Mwera (mkuu wa shule) alinifukuza form 2 kwa kukosa ada. Then nikarudishwa kufanya paper nkascore div 1 (mwaka 2010). Nikarudi mtaani mwaka 2011 kutafuta Ada bila mafanikio, nikajisomea kiom om ila weekend.

Nililazimika kwenda kuandika notes kwa marafiki na kujadiliana. Nilisoma hivyo mwaka mzima mpk 2012 mwezi wa 3 shule yetu ikapata mkuu mpya wa Shule (Mwera alihamishwa). Nilivyosikia hivyo, nikamfuata mkuu mpya na kumueleza adhima yangu ya kufanya mtihani wa F4
Nilijua fika hawez kuniruhusu kusoma bure ila mtihani atakubali. Nikasema liwalo na liwe In @gracemella95 voice . Baada ya mwezi1 nakumbuka tarehe 29/4/2012 Mwl. Banda (mkuu) kaniita na kuniambia niendelee na shule ila cheti sitachukua mpaka nimalizie ada. Nikafurahi sana Kama @samagoaI_77 Nilisoma kama kichaa, kwakuwa ni last chance huku Mama mdogo akinisapoti msosi (nampenda Sana). Nakumbuka wenzangu wakienda kwenye michezo mie nasoma physics. Nilisoma kwa nguvu ili pia kumpa heshima mkuu na zaidi nifanikiwe, nilijifunza unyenyekevu Sana nisije mkwaza yeyote, Nikajituma mithili ya @mpambazi_ na sabuni yake.

Hatimaye tukafanya mtihani wa form 4 mwezi Nov 2012. Mwaka ule matokeo yalikuwa mabaya Sana na yalirudiwa kutangazwa mara mbili. Mara ya Kwanza nilipata 3 ya 22 ya pili nikapata 2 ya 20. Nilifaulu pekee kwenda form5. Nilishukuru Sana Mungu, wawezeshaji na mkuu kwani ndoto yangu ya kuwa Dr Kama drmabula ilianza kuonekana baada ya kubalance PCB. swali nililokuwa najiuliza, "NITASOMESHWA NA NANI"?

Wazo likanijia baada ya kukumbuka kitabu Cha Mama Ntilie akina pita wakafanikish mpk kupata sheraton hotel Ndipo wazo la kwenda machimbo ya Dapori(mpkani na msumbiji) likanijia. Kaka @MpondaSabinus anakufahamu. Kule kwetu Mbinga kijana akipigika kimbilio lilikuwa machimbo kutafuta maisha. Nilipambana haswa Kama @TunduALissu na Ccm. Lengo zikitoka post niweze kupata Ada ya PCB

Nikafika machimbo, nikapata kazi ya kubeba kuni na kokoto kuanzia Feb 2013 mpk June 2013. Nikiwa msumbiji nikapata taarifa post zimetoka na nimechaguliwa kwenda kusoma MBEYA SEC SCHOOL (PCB), hapo mfukoni nilikuwa na tsh 560,000 Kama mtaji. Nikarud om tar 11/7/2013 Kuja kusoma form Ada yake ilikuwa 75,000 tu lakin michango mingine ikafika 320,000. Tufupishe stori, nililipa Ada ya form 5 tu na maisha yakawa magumu nikarudishwa Tena om Sina Cha kufanya Tena (Safari hii nilikosa msaada kabisa) kipato Cha bro kilikuwa chini ya laki 4 tu 2014 April, nikarud Tena msumbiji machimboni. Safari hii mawazo ya kusoma PCB yalihama na kuamua nikasake pesa nirud kusoma chochote Cha msingi maisha yaende . Nikafanya kazi ya kokoto kwa miezi minne. Ndipo August 2014 nikawa na laki 435 Hv. Nikarudi mbeya na kusajili mtihani Kama mtahiniw binafsi huku nikisoma HGL Sasa kwenye tuisheni pale nyuma ya kabwe (SEBAMA). Ada ilikuw elf 25 kwa mwez hivyo nikalipa miezi 8 na Kodi miez 6 (12000 per month). Hapa nikatumia maarifa ya @RednetCompany juu ya asset na liabilities . Mwezi wa 5 2015 nikafanya paper Ndipo July 2015 matokeo yakayoka nimepata merit. Nikamshukuru Mungu kwakuwa nimefaulu nikajiona Kama mwanafalsafa "Muda mwingine sio lazima nipate ninachokitaka Bali ninachojaaliwa". Ndoto ya kutimba chuo ikawa mbichi, kwa hasira za mafanikio nikapanga malengo ya 10 years later Mwezi September nikapata taarifa nimechaguliwa chuo Cha SAUT- campas ya Moro (JUCO) Kusomea shahada ya Elimu. Na mkpo nikapata 100%. Nikawek agano jipy la uwekezaji kuanzia bum la 1. Ctk kurud ten machimbo . Hivyo nikafungua salon ya kiume mwez Nov 2015. Likizo nilienda nyasa

Kwa akina @efremngalekasr kununua samaki na kuuza ili kutimiza malengo, mwez wa 3 2016 nikapata Kama laki 9 za samaki na kuongeza saloon ya pili hapa Moro (tubuyu). Nikanunua boda2 na kumpa kijana kwa mkataba. Then hela ya field nikawekeza kwenye duka la vyakula Mwaka 2018 March baada ya kuona siku za kumaliza chuo zimekaribia nikawaza kuweka hatima Sasa. Wazo la kufungua tuition centre likanijia kwa uzoefu niliouona MBEYA. Ndipo nikasaka majengo na kuyapata ndani ya maonesho ya 88 Moro baada ya chuo Cha uandishi Morogoro kufilisika Nikafungua centre kwa jina la TANZANITE TUITION CENTRE. nikauza wazo kwa vijana wakaona halina maslahi then nikaenda kuuza baadhi ya raslimali zangu na kununua madawati, meza, computer, vitabu, kukarabati majengo na vifaa vingine vya ofisini. Nikaanza na wanafunz 7 hivi. Hao hapo Baada ya kuanza kazi na timu ya walimu 4 nikagundua kwamba ukanda huu hawapendi tuition centre ila open school. Ndipo nikaanza mchakato wa kusajili open school but TANZANITE ikashindikana kwakuwa jina lipo kwenye list. Ndipo nikabadili jina na kuita GREENLIGHT OPEN SCHOOL Nikapata na sare za wanafunzi. Nikapewa kibali Cha kutangaza shule na kufika June 2020 usajili ukakamilika. Idadi ya wanafunzi ikaanza kupanda kutoka 27 mpk 49 mwezi September 2020 na kati yao 8 wanasoma bure kulingana na Hali yao kuwa ngumu (kila nikikutana na mwanafunz wa hivyoNataman watoboe).

SASA KWANINI LEO MOYO WANGU UNAVUJA DAMU
Ni hivi, mwezi September 2020 nilipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha Kama mwenezi wa chama akaniomba nichangie milion 1 ya kampeni. Nilishtuka Sana.Nikamjibu taasisi yangu bado haina huo uwezo was kuchanga m1 kwa Sasa. Ukweli Ni kwamba tangu mwaka 2018 cjawah jilipa mshahara. Muda mwingine posho ya walimu naunga unga na nakumbuka niliuza pikipiki yangu mwezi July kulipa posho na uendeshaji wa Shule kutoka kwenye covid19 Yule Bwana kanitishia kwa kauli ngumu kwamba lazima nitoe. Lasivyo nitaona

Leo asubuhi mabwana afya wamekuja kukagua mazingira, wameulizia choo nikaonesha matundu 3 nikaulizwa idadi ya wanafunzi nikajibu 49. Nimeulizwa usajili nikaonesha cheti. Then nikaambiwa Matundu matatu hayatoshi na mazingira sio rafiki kwa Kusomea hivyo nilipe faini ya 2.5 milion kwa kukosa choo na nikichelewa mpaka j3 watafunga kituo kabisa. Nimejaribu kumpigia mkurugenz wa Elimu ya watu wazima kumweleza sijajibiwa kwa ufasaha.

Kwakweli nimepambana Sana kutafuta maisha na kuhakikisha natoboa pasipo kutegemea msaada kutoka popote. Hapa nimefika kwa jitihada nyingi mno, Mali zangu nyingi niliuza ili kusimamisha msingi huu mpya. Mpka muda huu moyo umeumia Sana na hii vita Ni kubwa mno Tena Sana.
Mimi Ni mtanzania
Nimesoma kwa shida
Ajira yao wakaninyima
Nikajiajiri mwenyewe
Nikaajiri na wengine
ili Watoto wapate elimu
Bado nafanyiwa nongwa tu
Uhuru wa kujiajiri uko wapi? Au mlivyositisha kutoa Ajira mlitegemea sisi tufanyeje? Si Bora mtunyonge tu Sasa.

Email: mapundagustaph@gmail.com
Cc
@Ms_Dahir @biturojr @Roma_Mkatoliki Bajabiri @esteramosbulaya Gillsaint @LusakoWaKwanza Kigogo2014 @mpambazi_ drmabula @MarekaMalili mkandamizaji adamlutta @gamutu_ @razaqdm01 @JemsiMunisi @Mkuruzenzi @rollymsouth @Semkae @FlavianaMatataView attachment 1596281View attachment 1596280View attachment 1596282View attachment 1596283View attachment 1596284
IMG_20201010_211520.jpg
 
Today is World's Mental Disorder Day
Close to 1 billion people have a mental disorder
-Depression is a leading cause of illness & disability
-1 person dies every 40 seconds from suicide
-3 million people die every year due to harmful use of alcohol

You, CCM Hooligan you are increasing this number unnecessarily
 
Usinge andika kwanza unge mnasisha kwa takukuru mzee baba ungempa hela za moto kwasababu stone kasema wasichukue rushwa na akijua anawatimua.
 
Kuna watu wanajiona wanamsaidia mkuu kumbe wanampotezea kura. Halafu unaweza kukuta hio 1m wanayodai ikasaidie kampeni wala haifiki huko kwenye kampeni!
 
Tunapoipinga ccm tunamaanisha, wewe ni mmoja kati ya mamia elfu ya vijana walioathiriwa direct au indirect na utawala dhalimu wa ccm.
 
Mwamba usikubali ulichokianzisha kife, watoto wataumia sana, fanya hv uwekezaji wako ni wa uhakika, najua umepitia magumu sana, kama nlivosema hapa Chanzo cha kutofautiana kiakili kwa binadamu ni nini?

Ushaur wangu ni bora uuze hiyo hatimiliki uhame eneo hilo, piga gharama zako umtafute mwanachama wa CCM umweleze yoteee yanayokusibu umuuzie

Yani wewe uwezi kujipendekeza, uwezi unafiki tanu mtoto ni mtu wa misimamo, sitoshangaa wakikuita mpinzani.

Sent from my TECNO KD6 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom