Moyo unaniuma sijui nifanyeje?

UTAUMIA UTALIA LAKINI MWISHO WA SIKU UTASAHAU NA UTAMPATA ANAAEKUFAA POLE SANA KIJANA SOMA KWA BIDII MAANA MKE MWEMA ATAPATIKANA KWA UKUBWA WA POCHI YAKO...ILA USIPOKUWA NA POCHI ILIYOTUNA UTAISHIA KUOA MKE ILIMRADI NA WEWE UONEKANE UMEOA.
 
duuuuu,unaishi dunia gani?
 
Miaka 19 bado unakuwa mzito kwenye maamuzi ya mapenzi? Nyie ndo mnaoishia kujinyonga
 
Dini siku hizi zimekuwa sehemu ya kuficha maovu. Eti ana hofu ya Mungu halafu ana wapenzi 4. How comes?
Mnadhalilisha sana Mungu wa wote. Kwenda kweny nyumba za ibada haimanishi kuwa una hofu ya Mungu.
Mkuu tulia, kuwa busy na masomo hayo yote yatakwisha na utayasahau.
Umenikumbusha kale ka msemo ka wazinzi '' Shetani alinipitia'' sasa ww umekaleta vice versa. Eti ana hofu ya Mungu lkn ana wapenzi 4 duh!
 
Sasa bro nakushauri kwamba huyo demu ni muongo na tena keshaliwa na kukunwa sana isipokuwa wewe umeingia kichwa kichwa na sasa anatingisha kiberiti,eti anataka aachane na nyie wote ili arudi kuwa binti wa kanisani,hii haingii akilini,mwambie hata wewe umepata mwingine na hutaki upate dhambi kwa sababu yeye ameamua kumrudia Mungu,hapo patakuwa patamuuuuuu hadi utakuja kunipa shukurani na utaamini mademu nuksi kwa kutikisa kiberiti,yaani uwe mkavu na umwambie kiume kuwa umempata mnaoendana kitabia na kimapenzi.Halafu kumbuka usicheze na elimu.
 
piga moyo konde na usonge mbele pia udumu katika maombi, michezo na ujichanganye na watu wengine. nothing is permanent not even our troubles, yatakwisha pia hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho Mkuu
You said it all....
Kingine zingatia masomo yako,build your dreams. Hujachelewa,start now..mapenzi hapo,tumeyakuta na tutayaacha.
 
Reactions: THT
nilikua naisoma habari ....nilipofika hapo Mimi sijui Nina miaka 19 ....baaaas
 
Wakuu naomba mtofautishi kati ya mungu na MUNGU,hayo ni maneno ma wili tofauti
 
Mashaka yangu pekee ni huu ya umri wenu ambao naona bado ni mdogo. Nahisi ni umri ambao hisia zina nguvu zaidi kuliko akili, kwa hiyo uthabiti wa kudumu katika mahusiano ni hafifu sana.

Ungekuwa walau 25 ningekushauri kuweka msisitizo mpaka umpate kwa kuwa umesema unampenda na anajheshimu. Nakuhakikishia kuwa hiyo binti anatumia mbinuya kusema anaachana nanyi wote ili kuona ni yupi kati yenu yupo serious na yeye. Kumbuka hats katika utungisho (fertilization) ni sperm moja tu kati ya mamilioni ndiyo inayofanikiwa kuingia kwenye yai. Hiyo ni ile iliyoweza kukimbia, kuvumilia na kupambana hadi mwisho.

Be that sperm. Never give up.Ni wale tu wansopambana na kuvumilia hadi mwisho ndio wanashinda.
 
Tumeongea tumeelewana nimemwambia simwachii hat a iweje
 
Sawa mkuu
 
simama katika kweli ya Mungu utapata majibu.
 
Unaijua GPA ya 3.5? Ukishaijua amua uendelee kuumwa moyo au ukomae na GPA ya huko college kwako..
 
Hahahahahaa UKWATA, CASFETA, MAPENDO DAIMA ya shule huku mtaani ni magumu. Kuna maisha halisi huku, mshike Mungu kisawasawa Sio kishule shule. Utakuja kuona kuwa hakuna investment ya hovyo Kama ya kwenye ngono!!! Hailipi kabisa aiseee, Wazuri wapo wengi sana, kwa umri wako kuwa na Mpango Mkakati na binti Wa mwenzio ni uchochezi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…