Moyo kuuuma.

Linamo

JF-Expert Member
Jan 12, 2011
9,976
24,490
Habari Jf doctor...Naombeni Masada katika hili.Nina mama mkwe wangu analalamika sana kupata maumivu ya moyo yani moyo unamuuma. Naomba kujua sababu na namna ya kulikabili tatizo hili.
 
hiyo kitaalamu inaiwa Angina (chembe ya Moyo).Kwa ushaur zaidi amuone mtaalamu wa mambo ya moyo!
 
hiyo kitaalamu inaiwa Angina (chembe ya Moyo).Kwa ushaur zaidi amuone mtaalamu wa mambo ya moyo!

Kaka unaweza kunisaidia maelezo kidogo ya Angima?? Ili nijue pakuanzia na matibabu yake.
 
Habari Jf doctor...Naombeni Masada katika hili.Nina mama mkwe wangu analalamika sana kupata maumivu ya moyo yani moyo unamuuma. Naomba kujua sababu na namna ya kulikabili tatizo hili.

Ugonjwa wa Moyo

Magonjwa ya moyo yamezidi siku hizi. Mishipa ndani ya moyo huweza kufungana kwa mafuta na kuleta mshituko wa moyo au kupooza.

Jinsi ya kuzuia ugonjwa wa Moyo:

Fanya mazoezi kila siku

Zingatia uzito wa wastani

Usivute sigara

Pima presha ya damu yako
Kula vizuri:

Matunda, maboga na nafaka.

Usile vyakula vyenye mafuta mengi. Hivi ni kama vyakula vimekaangwa ama vichopochopo

vilivyo na mafuta ya nazi.

Usile chakula kilicho na cholestoral nyingi. Cholestoral ni mafuta ya nyama na inakuwa kwa vyakula kama nyama, mayai, siagi na mziwa ya krimu.
Ishara za ugonjwa wa Moyo

Mgonjwa ale kwa wingi ndizi mbivu na maji ya uvuguvugu kwa wingi.

Jambo la huzuni ni kwamba, hutapata dalili zozote za ugonjwa wa Moyo mpaka wakati mishipa ya damu kwa moyo imezibika. Kwa hivyo, kuwa na ratiba ya kumuona daktari mara moja kwa mwaka ili akague moyo wako. Unapohisi uchungu kifuani hasa baada ya zoezi ngumu, haraka muone daktari.

Dharura! Labda unashambulizi la ugonjwa wa Moyo ukiwa na:

Uchungu kifuani

Maumivu ya kifua yanayo tambaa mikononi, mabegani, mgongoni na kadhalika

Shida kupumua

Kisunzi, kutapika na maumivu yanayosambaa tumboni.

Nenda hospitali kamuone Daktari.
 
Habari Jf doctor...Naombeni Masada katika hili.Nina mama mkwe wangu analalamika sana kupata maumivu ya moyo yani moyo unamuuma. Naomba kujua sababu na namna ya kulikabili tatizo hili.

Vipi ulishaenda hospitali?Linaweza kuwa ni tatizo la moyo,lakini inawezekana pia lisiwe tatizo la moyo.Magonjwa mengi yanaweza sababisha maumivu kifuani.Kama bado hujapata msaada wa daktari,niandikie pm nitakusaidia.Unaweza kuniandikia namba zako za simu kwenye pm pia,halafu nitakupigia na kukuelekeza cha kufanya
 
Back
Top Bottom