Moyo hauhusiki kabisa na kupenda/mapenzi

Moyo hauhusiki kabisa na kupenda/mapenzi

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,780
Reaction score
8,155
Na Einstein Thought

Imewahi kukutana na maelezo kama vile "Ninakupenda kutoka moyoni mwangu", au "moyo wangu umejawa na mapenzi kwaajili yako" au labda " Ninakupenda kutoka ndani kabisa ya kilindi au uvungu wa moyo wangu? ".
Maneno hayo hapo juu Kwa akili za kawaida na akili za wengi huisi Kuwa ni kweli moyo ndio unaohusika na shughuli zote za kupenda, lakini swali la msingi ni Kuwa je ni kweli moyo unahusika na kupenda? Jibu ni HAPANA.

Maelezo ya moyo kuhusika na mapenzi ni maelezo yaliyotolewa na jamii nyingi za kale kipindi Cha uhaba wa sayansi na teknolojia na zikipigiwa muhuri na maelezo ya dini ambayo kimsingi ni uongo na upotoshaji mkubwa.
Unaweza kujiuliza hivi hawa waandishi wa vitabu vyao vitakatifu hawakuongozwa na Mungu wao Kuwa moyo HAUHUSIKI na kupenda? Au ndio tuseme Mungu wao hakujua? Ok hebu tuachane na hayo kwanza, twende tujifunze ni kipi na kipi katika mwili wa mwanadamu kinahusika na kupenda.

JE NINI CHANZO NA SABABU YA UPENDO KATIKA MWILI WA MWANADAMU?
Swali hili linajibiwa kutoka katika makundi mkuu matatu yanayofanya kazi Kwa pamoja ambayo ni
1. Sayansi ya ubongo (Neuroscience)
2. Biolojia ya mwili na
3. Saikolojia
Kimsingi swala la upendo katika mwili wa mwanadamu ni jambo linalohusisha ubongo,biolojia, kemikali na hata saikolojia pia.
Ili kufupisha somo Leo nitazungumzia Kwa kugusa sehemu tofauti tofauti lakini zaidi nitajikita kwenye Neuroscience ambayo ndio msingi mkubwa wa upendo.

Upendo Kwa mwanadamu si jambo la kiroho au la moyoni kama wengi wenu mnavyoelewa, Bali ni jambo linalohusisha msingi wa kikemikali (chemical) katika ubongo na mwili mzima kama nilivyokwisha kusema.
Lakini pia Kuna vichocheo (hormones) na kemikali za neva (Neurotransmitter) zinazochochea hisia za upendo kutokea.

VITU VINAVYOSABABISHA HADI UNAPENDA NI

1. DOPAMINE
Hii ni kemikali ya neva (Neurotransmitter) ambayo huzalishwa katika ubongo hasa kwenye sehemu kuu mbili ambazo ni SUBSTANTIA NIGRA pamoja na kwenye VENTRAL TEGMENTAL AREA (VTA).
Lakini pia kemikali hii inatengenezwa kidogo kwenye Figo mbali na kwamba kiasi kikubwa huzalishwa kwenye Neva lakini kazi yake kuu inafanyika kwenye ubongo.
Kazi ya dopamine ndio hukufanya wewe kuhisi furaha na hisia nzuri hasa unapokuwa karibu na mtu Fulani. Ni dopamine hii hii NDIYO humfanya mtu kujisikia vizuri anapokuwa amepata labda chakula kizuri au amefanya ngono au labda kapata mafanikio Fulani.
Kemikali hii inapoachiwa humfanya pia mtu Kuwa na motisha wa kufanya jambo Fulani na pia kumfanya mtu Kuwa mwenye furaha.
Kemikali hii ikiwa chache Kwa mtu huweza kumsababishia magonjwa kama vile msongo wa mawazo tunaita depression, Ugonjwa wa parkinson's na hata ukosefu wa motisha.

2. Kitu Cha pili ni OXYTOCIN.
Hii ni homoni lakini pia ni neurotransmitter inayozalishwa kwenye ubongo hasa kwenye hypothalamus na kisha hutolewa na pituitary gland (Tezi ya pituitary). Homoni hii imepewa jina la homoni ya upendo (love hormone) au (bounding hormone) kutokana na kazi yake ya kuuhamasisha mwili katika matendo yanayotafsiriwa Kuwa ndio upendo.

Kazi kubwa ya Oxytocin si tu kuimarisha uhusiano wa kihisia pekee Bali pia huweza kumfanya mtu Kuwa mtulivu hasa anapokuwa na mtu Fulani ambae anamvutia.
Ni oxytocin inayohusika Kwa mama wakati wa kujifungua na pia humsaidia mama kutoa maziwa na kutengeneza hisia za muunganiko kutoka Kwa mama kwenda Kwa mtoto.
Oxytocin ikiwa chache inaweza kuleta shida ya mtu Kuwa na hisia na pia hata shida ya kunyonyesha Kwa mama.
Homoni hii huachiliwa Kwa wingi wakati wa kukumbatiana, kugusana au hata Kuwa karibu kihisia na hii ndio sababu mtu anajisikia vizuri sana anapokumbatia, kufanya ngono au hata kusikia maneno mazuri.

3. SEROTONIN (Kemikali ya furaha na utulivu)
Hii ni kemikali ya ubongo (Neurotransmitter) inayosaidia kusambaza taarifa Kati ya seli za neva (Neurons).
90% ya kemikali hii inazalishwa tumboni kwenye Gastrointestinal tract na 10% pekee ndio huzalishwa kwenye ubongo hasa kwenye eneo linaloitwa Raphe nuclei iliyopo ndani ya brainstem.

Kazi ya serotonin ni pamoja na kudhibiti hamu ya ngono kwani inapokuwa Kwa kiwango kikubwa huweza kumfanya mtu asiwe mwenye hamu ya ngono, lakini ikiwa katika Viwango vizuri humfanya mtu Kuwa katika Hali nzuri ya kuitaji na kufanya ngono.
Mtu akiwa na upungufu wa serotonin huweza kupatwa na matatizo kama vile msongo wa mawazo, wasiwasi, hasira za mara Kwa mara na kula sana au kukosa hamu ya kula. Hii ndio sababu watu wengi wenye msongo wa mawazo hupewa dawa zinazosaidia kuongeza serotonin mwilini, mfano SSRIs (Selective Serotonin Reuptake inhibitors)
Serotonin inapokuwa juu humfanya mtu kujisikia furaha na kujiamini.

4. PHENYLETHYLAMINE (PEA).
Hii ni Neurotransmitter inayozalishwa kwenye ubongo na hu deal sana na mapenzi ya mwanzoni.
Huachiliwa Kwa muda kisha huisha na Kuwa replaced na Oxytocin.
Wakati inaachiliwa kemikali hii humfanya mtu kupagawa kimapenzi, na hii ndio sababu watu wengi hupagawa sana kipindi Cha mwanzoni Cha mapenzi kwani kipindi hicho huwa inaachiwa kemikali hii, kisha huisha na Oxytocin huchukua nafasi yake.

5. OESTROGEN (TEZI YA KIKE)
Hii hupatikana maeneo ya tumboni jirani kabisa na kiuno , Tezi hii hufanya kazi nyingi pamoja na kumpa mwanamke hisia za kuitaji tendo, lakini pia kuongeza mvuto wa kimaumbile na mambo kadha wa kadha.

6. TESTOSTERONE (TEZI YA KIUME)
HII hupatikana chini ya uume katikati ya mapaja (Kwa wanaume pekee) na huusika na kuamsha hisia za mwili za kuitaji tendo,kuleta mvuto na mabadiliko mengine mengi ambayo hupelekea tamaa za kimapenzi.

KWA KUMALIZIA
Katika mchakato wote unaohusisha kupenda au mapenzi hakuna mahali popote pale ambapo moyo unahusika katika tendo linaloitwa kupenda. Isipokuwa wakati ubongo unatoa baadhi ya kemikali na homoni kama vile oxytocin ambazo huusika na kupenda homoni hizi huathiri mapigo ya moyo Kwa kuongeza mzunguko wa damu na hivyo kuufanya moyo udunde Kwa Kasi na kupandisha pressure ya damu, Jambo hili ndilo hufanya watu wengi wahisi Kuwa kitendo hicho Cha upendo kinafanyika moyoni.

Bila shaka umejifunza jambo Leo, sasa usiendelee kudanganywa tena na maelezo ya DINI zenu za kijinga Kuwa upendo unatokea moyoni.

ASANTE 🙏
 
Kuumia moyo kisa mapenzi ni kihehere chako tu KAZI ya moyo ni kusukuma damu na sio kubeba mizigo ya mapenzi
 
Mbona mie hivyo vyote sina, au sio binadamu wa kawaida?
Hadi nimeogopa kwa kweli. Woiiiiih
 
Back
Top Bottom