Movie: What happen to monday

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,443
20881930_1760719903970414_1377115846576464700_n.jpg


Muvi moja kali sana. Hebu itafute uone jinsi watoto mapacha saba wanavyoishi maisha ya kujificha tu ndani. Babu wao hakutaka wagundulike kwani wote wangeuawa na kubakizwa mmoja tu.

Wakati amewaficha, ili kutunza siri anawaambia kila mmoja atakuwa akienda siku ambayo ni jina lake. Wote walikuwa na majina ya siku, kuna Monday, Tuesday na siku nyingine. Wanaambiwa kwamba kwa lolote litakalomtokea mmoja, basi wengine nao litawatokea ili siri ifichwe.

Siku moja Monday alitoroka kwenda kucheza skatting, alipofika kule, akapata ajali kidole kikakatika, hivyo wote sita waliobaki wakakatwa kidole kile alichokatika Monday.

Wanakua wakubwa, nje anatoka mmojammoja kwa siku yake lakini watu wa nje wanahisi ni mtu mmoa kumbe ni watu saba tofauti ila wamefanana. Siku moja, Monday anatoka, harudi nyumbani, ilipofika Jumanne, inabidi Tuesday aende kuona nini kimempata ndugu yake, anapokwenda huko, naye harudi, anauawa.

Hilo linawachanganya wenzake, kila anayetoka, anauawa, mwisho wa siku wanabaki wanne, mmoja anajilipua nyumbani ila baada ya kufuta data zote kwenye kompyuta. Ni muvi kali sana...unaweza kujiuliza, kwa nini serikali iliamua kuwaua ndugu hawa mmoja baada ya mwingine? Hii muvi si mchezo, kuna huyo mmoja anaitwa Thursday, anapiga balaa japo hakumfikia Wednesday ambaye alipambana sana, mwisho wa siku akapigwa risasi ya kichwa ghorofani.

Hebu itafute. Mzigo wa mwaka huu huo.

Kama huna njoo uchukue Tandale.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom