Mourinho apumzike ukocha

changaule

JF-Expert Member
Jan 10, 2020
5,580
9,166
Nimejiridhisha pasi na shaka kwamba Mourinho mbinu zakee na mfumo wake umeshapitwa na wakati na kote anakotimuliwa huwa hawamuonei isipokuwa ni kweli hana uwezo wa kufundisha na kuongoza timu.

Kuanzia ajiunge na timu ya Roma, ameshinda mechi tano tu za ligi na kupoteza mechi tatu katika mechi nane.

Kwenye Europa league kashinda mechi mbili tu na jana kapokea kipigo cha mbwa mwizi cha magoli sita kutoka timu ya bodoe/ Glimt kutoka Norway.

Ni wakati sasa wa Mourinho kustafu ukocha maana hana uwezo wowote wa kufundisha timu
 
IMG-20211020-WA0032.jpg
 
Mbona unasema Mourinho tu kwanini sio ole gune au Ateta, mbona wanashindwa.
Hao uliowataja hawakuwa na uzoefu kwenye ukocha hivyo wapewe muda watafanya makubwa tu. Ole sio kocha aliyeshindwa mkuu, msimu ulioisha Manchester United wamekuwa washindi wa pili kwenye Europa league na pia amekuwa nafasi ya pili kwenye ligi kuu uingereza. Msimu huu kafanya comeback mbili matata sana vs vilareal na vs Atalanta. Ni basi imetokea watu wa Manchester United kutomkubale Ole
 
Kwahiyo ikachukua kombe gani?
 
Kwahiyo ikachukua kombe gani?
Anajenga timu mvumilieni tu mbona mnakuwa na moyo mwepesi hivyo? Ngoja amalize kujenga timu mtaona makombe yanayovyoongozana. Mjifunze kwa washabiki wa Arsenal walivyo wavumilivu
 
Familia yake utamlelea wewe? Unadhani kuwa jobless ni kitu kidogo? Muache mzee wa watu apuyange wee wamvunjie mkataba wenyewe wamlipe kiinua mgongo.
 
Anajenga timu mvumilieni tu mbona mnakuwa na moyo mwepesi hivyo? Ngoja amalize kujenga timu mtaona makombe yanayovyoongozana. Mjifunze kwa washabiki wa Arsenal walivyo wavumilivu
Kwahiyo wakati anajenga timu halipwi mshahara?
 
Kuna mkeka wa mtu umemwagikiwa na asidi kali sana 😂😂😂
 
Nimejiridhisha pasi na shaka kwamba Mourinho mbinu zakee na mfumo wake umeshapitwa na wakati na kote anakotimuliwa huwa hawamuonei isipokuwa ni kweli hana uwezo wa kufundisha na kuongoza timu. Kwanzia ajiunge na timi ya Roma, ameshinda mechi tano tu za ligi na kupoteza mechi tatu katika mechi nane. Kwenye Europa league kashinda mechi mbili tu na jana kapokea kipigo cha mbwa mwizi cha magoli sita kutoka timu ya bodoe/ Glimt kutoka Norway.

Ni wakati sasa wa Mourinho kustafu ukocha maana hana uwezo wowote wa kufundisha timu
Kwenye ligi ni wa tano, na kafungwa na timu ambazo kila mara zinaifunga Roma. Jana alianza na kikosi kibovu huku akiweka bench wachezaji muhimu kwa ajili ya game ya Napoli.
 
Back
Top Bottom