Moto wa korosho wakolezwa

Moto wa korosho wakolezwa

wandamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
510
Reaction score
839
*~ Korosho toka nje ya nchi zakatazwa*

*~ Kangomba yazidi kupigwa vita*

*~ Rais Magufuli apongezwa*

Na Mwandishi wetu, Mihambwe

Gavana Mihambwe Emmanuel Shilatu ameungana na wakazi wa Tarafa ya Mihambwe na Watanzania kwa ujumla kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwa uamuzi wake kununua Korosho zote kwa bei yenye maslahi kwa Wakulima.

*"Napenda kuungana na Mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais Magufuli kwa uamuzi mgumu aliouchukua wa kuamua kuwa upande wa Wakulima kwa kununua Korosho zote kwa bei maslahi kwa Mkulima. Ni uamuzi wa kihistoria na funzo kwa waliozoea kuwanyonya Wakulima wa Korosho"* - alisema Gavana Shilatu

Gavana Shilatu aliyasema hayo kwenye Mkutano wa Kata ulioshirikisha Vijiji na vitongoji vyote uliofanyika kijiji cha Namunda kata ya Mkoreha.

Katika mkutano huo, Gavana Shilatu alipiga marufuku uingizwaji wa korosho toka nchi jirani na ununuaji wa korosho kwa mfumo wa kangomba.

*"Narudia tena kuwasisitiza Serikali tunapiga vita vilivyo kangomba na hairuhusiwi hata kidogo kuingiza korosho toka nchi jirani. Ukikamatwa, utapata tabu sana"* alisema Gavana Shilatu.

Katika mkutano huo Gavana Shilatu alisikia kilio cha Wananchi walio wengi waliotaka kusomewa taarifa ya mapato na matumizi ambapo alitoa maagizo na pale pale mkutanoni Watendaji wa Vijiji na Kata walisoma taarifa za mapato na matumizi pamoja na taarifa ya miradi ya kimaendeleo.

Akiongea mara baada ya mkutano Mzee Mahmoud Juma aliisifu Serikali inavyochapa kazi ya kuwahudumia Wananchi.

*"Nampongeza Rais Magufuli na Serikali yake kwa kuchapa kazi na kutujali Watu wa kusini. Sisi wanyonge tunatamba awamu hii"* alisema Mzee Mahmoud Juma.
FB_IMG_1542378780992.jpg
FB_IMG_1542378784761.jpg
FB_IMG_1542378790065.jpg
IMG_20181116_105819.jpg
 
Zi
*~ Korosho toka nje ya nchi zakatazwa*

*~ Kangomba yazidi kupigwa vita*

*~ Rais Magufuli apongezwa*

Na Mwandishi wetu, Mihambwe

Gavana Mihambwe Emmanuel Shilatu ameungana na wakazi wa Tarafa ya Mihambwe na Watanzania kwa ujumla kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwa uamuzi wake kununua Korosho zote kwa bei yenye maslahi kwa Wakulima.

*"Napenda kuungana na Mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais Magufuli kwa uamuzi mgumu aliouchukua wa kuamua kuwa upande wa Wakulima kwa kununua Korosho zote kwa bei maslahi kwa Mkulima. Ni uamuzi wa kihistoria na funzo kwa waliozoea kuwanyonya Wakulima wa Korosho"* - alisema Gavana Shilatu

Gavana Shilatu aliyasema hayo kwenye Mkutano wa Kata ulioshirikisha Vijiji na vitongoji vyote uliofanyika kijiji cha Namunda kata ya Mkoreha.

Katika mkutano huo, Gavana Shilatu alipiga marufuku uingizwaji wa korosho toka nchi jirani na ununuaji wa korosho kwa mfumo wa kangomba.

*"Narudia tena kuwasisitiza Serikali tunapiga vita vilivyo kangomba na hairuhusiwi hata kidogo kuingiza korosho toka nchi jirani. Ukikamatwa, utapata tabu sana"* alisema Gavana Shilatu.

Katika mkutano huo Gavana Shilatu alisikia kilio cha Wananchi walio wengi waliotaka kusomewa taarifa ya mapato na matumizi ambapo alitoa maagizo na pale pale mkutanoni Watendaji wa Vijiji na Kata walisoma taarifa za mapato na matumizi pamoja na taarifa ya miradi ya kimaendeleo.

Akiongea mara baada ya mkutano Mzee Mahmoud Juma aliisifu Serikali inavyochapa kazi ya kuwahudumia Wananchi.

*"Nampongeza Rais Magufuli na Serikali yake kwa kuchapa kazi na kutujali Watu wa kusini. Sisi wanyonge tunatamba awamu hii"* alisema Mzee Mahmoud Juma.View attachment 936738View attachment 936739View attachment 936741View attachment 936745
Zidumu fikra za Mwenyekiti!!!!
 
Back
Top Bottom