Siku zote maendeleo mazuri hujitokeza na upande wa pili wake wenye kuumiza tena sana kwa baadhi ya wananchi.
Barabara hii kweli kabisa itakapoboreka kwa viwango vinavyokisiwa hivi sasa hata hao WENYE VIOSKI WABISHI watabaki wameduazwa jinsi gani wataalam wetu wa mipango miji walivyoona mbali sana katika kuliboresha jiji letu la Dar es Salaam, kuongeza kipato zaidi ya mara 100 kwa wafanyabiashara na kodi kwa serikali na mambo mengi kua murua zaidi ya hivi sasa.
Paamoja na yote nasema huu ndio wakati wa mfanyabiashara wa Tegeta aliyepata kujua maana ya BIMA KATIKA BIASHARA YAKE KUJIKINGA NA MAJANGA wao kuanza kutabasamu mpaka benki (la sio Benki ya NMB iliyoingia ukiritimbaa wa kutuzungusha zaidi na wagonjwa wetu na maiti za ndugu zetu pale Muhimbili) kwenda kujichotea kiulaiiiini.