Motivation serikalini

Jese Pinkman

JF-Expert Member
Mar 5, 2014
661
338
Habarini zenu, kwa wale wafanyakazi wa serikalini ni motivation ipi ambayo mnaipata mnapokuwa makazini ili kusudi perfomance ya kazi iongozeke?
 
Viongozi wa walimu ni waalimu wenzao. Tulitegemea wangejua uchungu ila mambo yamekuwa tofauti.
 
Motisha ni pamoja na posho, mafunzo kazini, kupandishwa mshahara, cheo, kupewa cheti cha utumishi Bora, pongezi

Upande mwingine, kupewa onyo la mdomo, la maandishi, karipio, kushushwa cheo n.k
 
Inategemea upo Idara gan kama mwalim hana motivation yoyote anafanya kaz tu kama ROBOT
Motivation ya Mwl nadhani anaipata baada ya kufanya kazi ya kusimamia na kusahihisha kitihani na pale seminar chache chache zitapotokea
 
Walimu wana opportunities nyingi sema hawazitumii: Ya kwanza ni access to market. Walimu wana monopoly ya soko la vitafunwa, chai nk kwa wanafunzi. Waalimu wana nafasi ya kujiendeleza kitaaluma huku mahahara unaingia n.k.
 
Watu wengi wanaichukulia serikali kama baba au ndugu ambako mnaweza badilishana hisia zenu. Serikali haina feelings. Ni mwajiri. Soma mkataba wako wa ajira kwa makini. Usimwazie vitu ambavyo havimo kwenye mkataba. Serikali inaweza kukuhamisha na kukupa siku 7 uwe umeriport kituo kipya kilomita 1000 bila kukuuliza mkeo na watoto wanafanya nini. Hawajakulipa nk.
 
mhh tunakoendea naanza kuona ni bora kufanya kazi private sector tena kwenye ngos zinazojielew,achana na ngos za kuwabagua wa tz na kuwalipa salary ndogo nazungumzia zile zinazojua principle ya equality kwny salary
 
Walimu wana opportunities nyingi sema hawazitumii: Ya kwanza ni access to market. Walimu wana monopoly ya soko la vitafunwa, chai nk kwa wanafunzi. Waalimu wana nafasi ya kujiendeleza kitaaluma huku mahahara unaingia n.k.
Mkuu wa KAYA kakataza kuuza hata kishet, hakuna tuition, hakuna kuchangisha mchango wowote shulen OLE wako ukikiuka Hilo ujue utafungwa.

Ukiwa nje ya system unaweza ukasema WALIMU wanafursa nyingi Lakin Co kweli kama unavyodhani.

WALIMU wanadhalilika sana asee mshahara unaisha tareh 5 tu.

WALIMU wanataabika jaman huko MAPORINI.

# ADUI WA MWALIMU NI MWALIMU MWENZAKE #
 
Kama wewe sio mtu wa kujipendekeza ili uonwe na wakubwa kama wanavyofanya wenzetu hapa jf hadi kukwaa uDC, hata kama unachapa kazi kisawasawa usitegemee kupewa motivation serikalini hasa huku kwenye halmashauri!
Haya nimeyaona kwa macho yangu, sijisifii kama ni kazi mimi ni kiboko( jina langu linavuma hadi vijiji vya mbali). Baada ya kuona utumishi wangu uliotukuka hauthaminiwi na wakubwa zangu sasa nimekuja na plani hii:nitawahudumia wananchi kwa nguvu zangu zote huku nikijiandalia mazingira ya kugombea udiwani mwaka 2020 hata kama ni kupitia UDP :rolleyes::rolleyes::rolleyes:
 
Back
Top Bottom