Motisha kwa wanaotaja wakwepa kodi

nyendo kintu

Member
May 31, 2011
20
2
Ndugu wanajamvi jana nimesoma post hapa kuwa nchi yetu inakalibia kufikia kiasi cha kutokopesheka kutokana na inavyokomba pesa kwenye taasisi za fedha! Maskini Mkwele! Napenda kuuliza hapa kwetu kuna sheria inayomlinda raia mwema pindi atoapo taarifa za watu wanaokwepa kodi? na sheria ikoje? maana nimechoka kuona watu hawalipi kodi na wanaikosesha serikali mapato mengi japo na magamba wataziiba! bila kusahau ni motisha kiasi gani inatolewa kwa kodi itakayokuwa recovered. Tusikate tamaa 2015 tutalinda kodi zetu wenyewe maana magamba hoi.
 
Ndugu yangu,unadhani tatizo ni kukwepa kodi? Kama ni hvyo mbona kla siku tra wanasema wamevuka malengo ya ukusanyaji? Tatizo hapa ni too much misamahaz manake tunasamehe hata wasostahili na hata hicho tunachokusanya tunaktumiaje? kwa kusafiria dunia nzima kuomba misaada? Kwa kulipana posho kama walivyofanya kina ngeleja,malima na jairo wao? Kwa kulipa wataalam wa kichina waje kufundisha alaiki watoto wetu? Au kuandaa sherehe kuuuubwa leo kumbe kesho huna hata mia ya kununua maji ya kunywa? Wazo lako ni zuri kakin tuangalie kwanza sera zetu,mipango yetu na matumizi yetu
 
Hata watoe mamilioni ya pesa,siwezi kuwataja kwani matumizi ya pesa ya kodi yamekuwa mabaya sana,ukiangalia na swala zima la kujiongezea posho kwa wabunge hlf mimi mwananchi wa kawaida naendelea kukalia kuti kavu!
 
Tatizo sio wakwepa kodi tu,hicho kingi kinachopatikana kinatumika vipi ?
Kuna ubadhirifu mkubwa wa mapato ya serikali. Kama kuna upungufu wa mapato kulikuwa na haja gani ya mbwembwe za uhuru,haya ma vx,gx,bmw,benz,discover a.k.a SU na STK, yanatoka wapi kama tax evasion ndo tatizo peke yake.
Kupanga ni kuchagua ,tunahitaji kuwa na mipango thabiti ya ukusanyaji na matumizi sahihi ya mapato. Tukikusanya halafu zikaishia kwenye posho,posh cars,na other unneccessary expenditure hata mimi siwezi kuwa na moyo wa kutaja wakwepa kodi bali nitatafuta njia za kukwepa. Maisha ni magumu, kwa nini uzibe kwa wengine wakati kwako panavuja.
 
Back
Top Bottom