Moshi tunahitaji madaraja ya watembea kwa miguu.

Moshi tunahitaji madaraja ya watembea kwa miguu.

TheChoji

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Posts
6,767
Reaction score
20,870
Katika kuendelea kuupendezesha mji wa moshi, naona kuna dosari inaanza kujitokeza. Hii inatokana na watu wanaovuka barabara kuongezeka sehemu nyingi hivyo kusababisha kuwekwa zebra kila mahali kitendo kinachoongeza foleni. Kwa sasa tatizo sio kubwa sana ila ni bora kuliwahi kwa kuweka simple pedestrian overpasses baadhi ya maeneo. Maeneo nayopendekeza ni

1. Mbele ya kanisa la Kristo Mfalme

2. Stendi kuu eneo la double road (karibu na msikiti)

3. Eneo la kahawa house double road mkabala na posta

4. Stendi kuu upande wa KKKT zinapopaki hiace za KCMC

Kwa kuanzia nadhani maeneo hayo itasaidia sana. Asanteni
AAB52291-168C-4D9B-8ECB-57AFD0B1C11E.jpeg
4BEDEC87-98D6-4683-803C-CE437792EC9A.jpeg
 
Mkuu alisema kaskazini msubiri kwanza hivyo hamjaelewa?
 
Jiwe alisema kaskazini msubiri kwanza hivyo hamjaelewa?
Hata mambo madogo kama haya Jiwe anahusika? Mbona naona barabara zinajengwa? Hivi ni vitu vidogo sana wala jiwe hana haja ya kujua..
 
Hicho kimanisipaa cha moshi mna viherehere sana.

Dodoma imewakuta na kuwaacha mkipiga domo mitandaoni eti mmeendelea
 
Back
Top Bottom