MOSHI : Polisi Line wanaishi gizani kwa kukosa umeme mwezi mzima sasa kwa deni la 1 Bilion

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Polisi na familia zao wanaoishi katika kambi maarufu Police Line, wanaishi gizani kwa mwezi mzima sasa baada ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuwakatia nishati hiyo kutokana na malimbikizo ya madeni.
Baadhi ya polisi waliozungumza na gazeti hili jana walidai uongozi wa Polisi mkoani Kilimanjaro, umewataka wenye uwezo wa fedha wafungiwe mita zao za Luku kwa Sh321,000 na watarudishiwa.



Hata hivyo, askari hao wanataka wapewe hakikisho la maandishi kuwa watarudishiwa fedha hizo na Serikali kwa vile utaratibu uliopo ni kuwa mita hizo zitasajiliwa kwa jina la RPC Kilimanjaro.
“Kambi ilipokatiwa umeme mazungumzo kati ya viongozi wetu na Tanesco yalifanyika na ikakubaliwa umeme urudishwe kwa kufungiwa mita za Luku wakati mazungumzo yakiendelea,” alidai askari mmoja.



Chanzo hicho kilidokeza kuwa kila upande katika pande tatu za kambi hiyo, ulifungiwa Luku na kuwekewa uniti 250, ziliisha ndani ya saa tatu kutokana na kambi hiyo kuishi familia zaidi ya watu 1,000.
Kwa wiki moja sasa, gazeti hili limekuwa likipita katika nyumba zilizopo katika kambi hiyo na kukuta giza tororo isipokuwa kwa maofisa wa polisi wachache waliomudu kufunga umeme wa jua.



“Tunaiomba Serikali itufungie hizo mita kwa gharama zao au kama kuna wenye uwezo basi wafunge lakini zisajiliwe kwa majina yao ili mwisho wa siku waweze kuhama nazo ikitokea,” alidai.
Polisi mmoja mwenye cheo cha sajini, alidai kitendo cha kukaa gizani licha ya jukumu zito wanalolifanya la kuhakikisha ulinzi wa raia na mali zao, limewaathiri kisaikolojia.



“Sasa hivi huwezi kuamini tunakwenda kazini na sare ambazo hazijanyooshwa. Tunamuomba Rais (John) Magufuli aingilie kati kwa sababu tunaumizwa tusiohusika,” alieleza polisi huyo.
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Hamis Issah, jana alithibitisha kambi hiyo kukatiwa umeme na kwamba ni zaidi ya mwezi mmoja na wanasubiri Serikali iwaunganishie umeme kwa mita za Luku.



Mwezi uliopita, Tanesco walitangaza kuanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli la kuzikatia umeme taasisi za Serikali, kampuni binafsi na watu waliolimbikiza madeni yanayofikia Sh3 bilioni.
Naye meneja wa Tanesco mkoani Kilimanjaro, Mahawa Mkaka alisema Polisi pekee inadaiwa zaidi ya Sh1.1 bilioni kikiwamo kituo cha Polisi Himo.



Pia, katika operesheni hiyo, Tanesco wamewakatia umeme Magereza waliokuwa wanadaiwa zaidi ya Sh400 milioni, lakini walirudisha huduma baada ya kuingia makubaliano ya kulipa deni hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo utaratibu upo nchi nzima kama kota zimewashinda wahamia kwenye nyumba zao mtu ana staafu hata kibanda hana, Na sio wao tu hata Magereza Na Majeshi mengine hakuna Umeme wa bure na Majeshi mengi tu saivi yana mita za Luku, idara ya maji nao waanze tu kuwafungia mita mana wanatumia tu maji free, Maneno ni Mawili KA na TA
 
Back
Top Bottom