TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Hakika Raais Magufuli,
Ni kiongozi na mtu mwenye akili sana kwa sababu husema kwamba hayuko tayari kumteua Mpinzani kuwa Mbunge lakini yupo tayari kumteua Mpinzani ktk nafasi nyingine kama ukuu wa mkoa nk.
JE, UNAJUA KWA NINI ANAFANYA HIVYO?
Sababu ni moja tu na yenye nia njema ndani yake; Kwamba hateui Wapinzani kuwa wabunge kwa sababu Ukishamteua mtu kuwa Mbunge huwezi Kumwondoa wala kumfukuza au kumwachisha kazi ya ubunge pale anapoenda kinyume na matarajio yako wewe uliyemteua lakini ukimteua mtu kuwa Mkuu wa Mkoa au Katibu Mkuu, au Mkuu wa Wilaya nk, ni kwamba wakati wowote unaweza kuwondoa ktk nafasi uliyotompatia.
Ktk muktadha huo ni wazi Rais Magufuli kafikilia mbali sana kuwateua wapinzani ktk nafasi ambazo wakienda kinyume anaweza kuwaondoa fasta. Ukishampatia Ubunge huwezi kumwondoa kiurahisi. Ni wazi Rais Mafufuli anaona mbali mnoo. Wasiokubaliana na hilo warejee wafuatao waliowahi kuteuliwa na Rais Kikwete baadaye waliifanya nini serikali yake ndani ya Bunge: Mhe Mbatia na Mhe Ismail Jusa? Nadhani kuna wakati Rais Kikwete alikuwa akijuta kuwateua watu hao kwa sababu waliipiga sana serikali na chama cha mapinduzi.
Heko Rais Magufuli kutowateua Wapinzani ktk nafasi za Ubunge na kuwateua ktk nafasi ambazo waweza kuwaondoa kiurahisi pale wanapoenda kinyume na matarajio yako. Lakini pia Umedhihirisha kuwa wewe siyo mbaguzi kwa sababu ya Itikadi za vyama bali unaangalia uwezo na uadilifu wa watu. Hakika wewe ni kiongozi makini.