Morogoro: Waziri Lukuvi arejesha ekari 9,000 kwa wananchi wa Ulanga

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
Juni 11, 2016

Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mhe.Wiliamu Lukuvi ametwaa hekari elfu 9 kati ya hekari elfu 49 za ardhi iliyokuwa inamilikiwa na muwekezaji wa kampuni ya Karangamiti katika kijiji cha Chita wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro na kuigawa kwa wananchi 764 wa kijiji hicho.

Hatua hiyo ya waziri Lukuvi kurejesha ardhi hiyo kwa wananchi imekuja baada ya malalamiko ya wananchi ya muda mrefu ya eneo hilo kutoendelezwa na muwekezaji huyo kwa zaidi miaka 20 huku wananchi hasa vijana wakiendelea kusota kwa kukosa maeneo ya kilimo.

Waziri Lukuvi akiwa katika muendelezo wa ziara yake mkoani Morogoro kwa lengo la kukagua na kujiridhisha juu ya malalamiko ya wananchi kuhusu mashamba pori yanayomilikiwa bila kuendelezwa.

Akijitetea mbele ya waziri Lukuvi mwakilishi wa mwekezaji huyo Bi Luose Ngugi raia wa nchini Kenya amesema sababu ya kulitelekeza shamba hilo ni kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mibovu licha ya kuwa amekwisha anza ujenzi wa kituo cha kiliniki katika kijiji hicho.

Chanzo: ITV
 
Mwenye mamlaka ya kutwaa ni rais baada ya kushauriwa na kamishna mkuu wa ardhi...kwa hiyo lukuvi angesema rais kaagiza ,,na kwamba yeye katumwa tu....kwenye ardhi waziri ana katone tu ka mamlaka,trustee yuko magogoni
 
Back
Top Bottom