Morogoro: Watu 22 wahukumiwa kifungo cha miezi 6 jela kwa uzururaji na kujihusisha na biashara ya ngono

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mahakama ya Mwanzo Nunge manispaa ya Morogoro imewahukumu watu 22 kifungo cha miezi sita jela baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la uzembe na uzururaji.

Baada ya hakimu Emelia Mwambagi kusoma hukumu hiyo, washtakiwa hao ambao wengi ni wanawake waliangua kilio mahakamani, kuomba kusamehewa.

Kesi hiyo ilisikilizwa jana Jumatano Agosti 28, 2019 kwa zaidi ya saa tano dhidi ya wasichana wanaodaiwa kufanya biashara ya ngono pamoja na wanaume wanaodaiwa kujihusisha na ushoga.

Washtakiwa hao walikamatwa usiku wa Agosti 16, 2019 eneo la Kahumba manispaa ya Morogoro.

Hakimu Mwambagi aliieleza mahakama hiyo kuwa adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa washtakiwa hao na wengine wanaotumia miili yao kujidhalilisha na kuwadhalilisha wazazi, ndugu na jamaa kwenye maeneo wanayotoka.

Hakimu Mwambagi aliieleza mahakama kuwa washtakiwa wote waliokamatwa ni vijana wenye uwezo wa kufanya kazi za kuwaingizia kipato halali lakini wamekuwa wakizurura na wengine wakitumia vibaya miili yao.

Kabla ya kutoa hukumu hiyo hakimu Mwambagi aliwaachia huru washtakiwa sita kutokana na utetezi wao pia vielelezo walivyoviwasilisha mahakamani hapo kudhihirisha kuwa hawahusiki na shtaka hilo.

Katika utetezi wao washtakiwa hao walidai walikamatwa kwenye nyumba za kulala wageni walipokwenda kujipumzisha baada ya kutoka safari, huku wengine wakidai kukamatwa katika maeneo yao ya kazi wakidai kuwa wanajihusisha na biashara ya kuuza chakula.
 
Umesoma mpaka mwisho? Au ndo yale mambo ya mfiche Mtanzania kwa maandishi!?
Tanzania imefikia stage kuzurura ni kosa kisheria!??? au mimi sijaelewa maana hapo naona hukumj mbili moja ya kuzurura na nyingine kujihusisha na biashara ya ngono
 
Umesoma mpaka mwisho? Au ndo yale mambo ya mfiche Mtanzania kwa maandishi!?
hebu nifafanulie aya hii inamaanisha nini maana naona swali langu hujalijibu unataka nisome mpaka mwisho ili iweje sasa.....

"Mahakama ya Mwanzo Nunge manispaa ya Morogoro imewahukumu watu 22 kifungo cha miezi sita jela baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la /uzembe/na /uzururaji/."
 
Mahakama ya Mwanzo Nunge manispaa ya Morogoro imewahukumu watu 22 kifungo cha miezi sita jela baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la uzembe na uzururaji.

Baada ya hakimu Emelia Mwambagi kusoma hukumu hiyo, washtakiwa hao ambao wengi ni wanawake waliangua kilio mahakamani, kuomba kusamehewa.

Kesi hiyo ilisikilizwa jana Jumatano Agosti 28, 2019 kwa zaidi ya saa tano dhidi ya wasichana wanaodaiwa kufanya biashara ya ngono pamoja na wanaume wanaodaiwa kujihusisha na ushoga.

Washtakiwa hao walikamatwa usiku wa Agosti 16, 2019 eneo la Kahumba manispaa ya Morogoro.

Hakimu Mwambagi aliieleza mahakama hiyo kuwa adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa washtakiwa hao na wengine wanaotumia miili yao kujidhalilisha na kuwadhalilisha wazazi, ndugu na jamaa kwenye maeneo wanayotoka.

Hakimu Mwambagi aliieleza mahakama kuwa washtakiwa wote waliokamatwa ni vijana wenye uwezo wa kufanya kazi za kuwaingizia kipato halali lakini wamekuwa wakizurura na wengine wakitumia vibaya miili yao.

Kabla ya kutoa hukumu hiyo hakimu Mwambagi aliwaachia huru washtakiwa sita kutokana na utetezi wao pia vielelezo walivyoviwasilisha mahakamani hapo kudhihirisha kuwa hawahusiki na shtaka hilo.

Katika utetezi wao washtakiwa hao walidai walikamatwa kwenye nyumba za kulala wageni walipokwenda kujipumzisha baada ya kutoka safari, huku wengine wakidai kukamatwa katika maeneo yao ya kazi wakidai kuwa wanajihusisha na biashara ya kuuza chakula.
Japo siungi mkono utendaji wa makosa ambayo wametuhumiwa nayo kuyatenda, lakini Mahakama husika ingewapa adhabu mbadala kama vile kutozwa faini, na endapo kama kungekuwa na ulazima sana wa kuwafunga jela basi wangehukumiwa kifungo cha nje ili wangepata nafasi ya kuihudumia jamii.
Sambamba na hili, pia nashauri Mahakama ianze kufikiria namna ya kuwapa adhabu mbadala kwa Watuhumiwa wa vijikesi vidogo vidogo vya kipuuzi kama hivi.Mimi natamani kuona kuwa watu wanaofungwa gerezani ni wale tu ambao kwa hakika wanastahili kuwepo kwenye magereza kutokana na makosa yao waliyotenda kuwa serious.
 
Kwa Kosa la Uzembe na Uzururaji..dah kumbe Uzembe ni kosa kisheria eeh..bora kukaa ndani tu kuliko kuzurura..

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Gairo
 
Kutumia vibaya miili yao.....miili yao, miili yao....yaani ni miili yao.
Unajua baadhi ya Sheria zetu kwa kweli ni za kipuuzi sana, yafaa kuzikataa. Hivi MTU mzima mwenye akili zake timamu kuamua kuutumia mwili wake mwenyewe kwa namna hiyo kama biashara/bidhaa, na mnunuzi kwa hiyari yake akajitokeza kununua bidhaa hiyo; hivi hapo kuna kosa gani? Endapo kama wangelazimishwa au kuwalazimisha watu wengine kujihusisha na biashara yao, kwa kweli hapo ingekuwa kosa au tatizo, lakini kama wameamua wenyewe kwa hiyari yao wakiwa na akili zao timamu sioni kama kuna tatizo hapo.
Inavyoonekana kama vile Jeshi LA Polisi limekosa kazi ya maana ya kufanya.
 
Mambo kama haya ndiyo yanafanya waafrika tuonekane ni sawa na mavi. Uzururaji ndiyo kosa gani? Sheria hii iliwekwa na mkoloni wakati huo kwa maslahi ya mkoloni. Sisi sababu ni mavi tunachukua kila kitu na hatufanyi maboresho. Mbwa kabisa kiumbe mweusi.
 
Wazurulaji wakubwa ni pamoja na hao mahakimu, kazi kubwa ni kuahirisha kesi na kwenda wanakojua. Hatuna hali ya hatari nchini inayozuia watu kutembea usiku, hatuna sheria ya kumzuia mtu kuingia guest. Ni ukiukaji haki, ni ubabe.
 
Tayari wametengeneza scarcity ya madada poa,tugemee mfumuko wa bei hapo Morogoro.

Naona wengi wamesombwa kutoka Kahumba! Sasa mhamie Samaki Samaki ambako nasikia wana unafuu zaidi kwenye suala zima la usafi kuliko wale wa Kahumba na Itigi msamvu.
 
Back
Top Bottom