beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,879
- 6,356
Wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha sukari cha Ilovo kilichopo wilayani Kilombero na Kilosa mkoani Morogoro wametishia kusimamisha uzalishaji na kuzima mitambo ya kiwanda hicho, iwapo menejimenti itaendelea kukataa mapendekezo ya wafanyakazi ya kuongeza kiwango cha mshahara kwa zaidi ya asilimia 15 badala ya asilimia 2.2 iliyofikiwa na mwajiri baada ya kuvutana kwenye vikao kwa muda mrefu.
Hatua hiyo imefikiwa katika maazimio ya wafanyakazi wa Ilovo waliokutana kiwandani hapo,ambapo mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wa mashambani na kilimo Tpawu Isack Magassa amesema wamekutana katika vikao mbalimbali vya kujadili nyongeza ya mshahara bila mafanikio,ambapo mwajiri alikataa mapendekezo ya nyongeza hiyo akifikia asilimia 2.2 tu tofauti na mapendekezo ya sheria ya nyongeza isiyozidi asilimia 25.
Awali baadhi ya wafanyakazi waliokuwa na mabango ya kueleza malalamiko yao, wamelia na changamoto mbalimbali ikiwemo kwa baadhi ya viongozi wazawa kuwanyanyasa badala ya kuwatetea, mwajiri kuajiri wafanyakazi wa nje ya nchi wasio raia 22 wanaofanya kazi zinazoweza kufanywa na raia wandani, mshahara duni, upendeleo na rushwa katika ajira.
Afisa utumishi wa Ilovo Tatu Mgonde aliyehudhuria kikao hicho alikataa kuzungumza lolote kwa madai kuwa menejimenti inafahamu changamoto zilizotajwa na ndio maana imeruhusu uwepo wa kikao hicho, lakini mbunge wa jimbo la Mikumi, Joseph Haule, akaahidi kupeleka changamoto hizo katika mamlaka husika.