figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,689
- 55,661
Wananchi wa kijiji cha Bunduki kata ya Bunduki tarafa ya Mgeta wilayani Mvomero,Mkoani Morogoro wanalazimika kutumia tochi na vibatari wakati wa kupata huduma nyakati za usiku katika zahanati ya kijiji hicho, baada ya Betri inayowezesha kupatikana umeme wa Jua kuharibika na kukosa nishati hiyo.
Wakizungumza kwenye mkutano wa kijiji baadhi ya wananchi Padrisia Benard na Monica Alex wamesema tatizo hilo limedumu kwa muda mrefu ingawa tayari umeme umefika kwenye zahanati hiyo,jambo linalohatarisha usalama wa mgonjwa na mtoa huduma nyakati hizo za usiku.
Wameutaka uongozi wa kijiji hicho na kata ya Bunduki kwa ujumla kufuatilia na kuhakikisha kero hiyo inatatuliwa ili kunusu maisha ya wagojwa na watoa huduma katika eneo hilo.
Afisa mtendaji wa kijiji cha Bunduki Evarist Kingungwi amekiri kuwa kero hiyo ni ya mrefu ingawa jitihada mbalimbali zimefanywa kuitafutia ufumbuzi bila mafanikio na kwamba awali walikuwa wakitumia wa umeme wa nishati ya jua lakini ulikosekana baada ya betri ya mfumo huo kuharibika.
Aidha Diwani wa kata ya Bunduki Prosper Mkunule amesema nishati ya umeme kwenye vituo vya afya na zahanati ni muhimu sana kutokana na wananchi kutegemea huduma katika vituo vya afya wakati wowote na kwamba matumizi ya tochi na vibatari yanahatarisha maisha na kukatisha tamaa kwa wagojwa na watoa huduma.
Mkunule amewahakikishia wananchi wa kata hiyo kutoa ushirikiano wa kutatua kero hiyo ya ukosefu wa umeme kwa kuwa tayari kulipia gharama zozote za umeme pindi zoezi hilo litakapo kamilika.
Chanzo: ITV