Agent-47
JF-Expert Member
- Mar 18, 2014
- 783
- 2,780
Treni za SGR zilizokuwa zikisafiri jioni ya leo kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma na Dodoma kwenda Dar es Salaam zimepata hitilafu na kulazimika kusimama njiani, hali iliyosababisha sintofahamu kubwa kwa abiria.
Kwa mujibu wa taarifa za moja kwa moja kutoka kwa abiria walioko njiani, treni hizo zimekwama maeneo ya karibu na Morogoro kwa muda mrefu bila maelezo ya kina. Abiria wamesema kuwa walitangaziwa kuwa “njia imepata hitilafu,” na hivyo safari ikasitishwa kwa muda.
Kutokana na changamoto hiyo, abiria wa treni zote mbili wamelazimika kubadilishana treni, ambapo waliokuwa wakielekea Dar es Salaam wameshushwa na kupandishwa treni iliyokuwa ikielekea Dodoma na vivyo hivyo kwa upande wa pili.
Hadi muda huu, abiria wanasema walipaswa kuwa wamefika Dodoma kuanzia saa tano, lakini bado wamekwama bila taarifa rasmi ya kinachoendelea, hatua inayoongeza hofu na usumbufu mkubwa kwa wasafiri.
Abiria wanaendelea kusubiri maelezo zaidi kutoka mamlaka husika kuhusu chanzo cha hitilafu na muda watakaoweza kuendelea na safari zao.