Morogoro: Mwalimu wa elimu ya awali anahitajika

Morogoro: Mwalimu wa elimu ya awali anahitajika

Joined
Nov 19, 2015
Posts
6
Reaction score
2
attachment.php

Karibu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Plot No. 214, Boma Road
P.o. Box 4664 Morogoro, TANZANIA.

Simu: 0783400701/0714022038
Barua Pepe: Happyvalleyschools@gmail.com
Tovuti:www.happyvalleyschools.blogspot.com



TANGAZO LA NAFASI YA KAZI


Happy Valley Day Care Center iliyopo Morogoro mjini karibu na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro inatangaza nafasi (1) ya kazi ya mwalimu wa elimu ya awali.

Majukumu ya mwalimu wa awali yatakuwa yafuatayo


  • [*=center]Kuwapokea watoto wafikapo shule na kuhakikisha wamerudi salama majumbani mwao
    [*=center]Kuwafundisha watoto elimu ya awali
    [*=center]Kuwahudumia watoto katika mahitaji yao mbalimbali
    [*=center]Kuandaa michezo ya watoto na kuwasimamia wanapocheza
    [*=center]Kutoa taarifa za watoto kwa wazazi kupitia shajara /diary za watoto
    [*=center]Kuhakikisha usalama wa watoto wakati wote
    [*=center]Kuhakikisha usafi wa watoto wakati wote
    [*=center]Kuandaa ripoti za mitihani za watoto.
    [*=center]Kufanya kazi nyingine yoyote ile inayoendana na taaluma ya elimu ya awali atakayoelekezwa na mkuu wake wa kazi.

Sifa za Muombaji


  • [*=center]Awe anapenda watoto
    [*=center]Awe angalau na cheti cha ualimu wa elimu ya awali kutoka chuo kinachotambulika
    [*=center]Awe na uwezo wa kuongea na kuandika kwa ufasaha lugha ya Kiingereza na Kiswahili
    [*=center]Awe na umri usiopungua miaka (25)
    [*=center]Awe mbunifu katika kuandaa michezo ya watoto
    [*=center]Awe na ujuzi wa kuwaelewa watoto kwa haraka
    [*=center]Awe na uwezo wa kujituma kuliko kuamrishwa
    [*=center]Mwenye uzoefu wa kufundisha watoto atapewa kipaumbele
Tuma maombi yako kupitia anwani ya barua pepe (E-mail) inayoonekana hapo juu. Pamoja na barua yako ya maombi, ambatanisha CV yako na nakala za vyeti vyako. Mwisho wa kutuma maombi ni tar 1/12/2015. Kwa maelezo zaidi piga kupitia namba za simu zinaonekana hapo juu.




 

Attachments

  • logo.jpg
    logo.jpg
    280.1 KB · Views: 401
Back
Top Bottom