Niko Morogoro kwa zaidi ya wiki moja sasa, hali ya hewa ni tofauti kabisa na ilivyokuwa miaka kumi na tano nyuma. Nakumbuka wakati ule muda kama huu hakukuwa na joto kiasi hiki, Hali ya hewa ilikuwa ni ya u baridi na mawingu mengi, Jua na humidity havikuwa kama ilivyo sasa. Kama ni mabadiliko ya tabia nchi basi Morogoro yajidhihirisha kabisa. Wadau/wenyeji wa Morogoro hii hali imeanza lini.

Na hii tabia ya watu wa manispaa ya Morogoro itaendelea kuwatia hasara kama haitabadilishwaHiyo sio tabia nchi nadhani ni tabia mkoa
Sasa kunguru na mafuriko, ukosefu wa maji na joto kipi bora? Kunguru wanadhibitika mfano Dar es salaam kunguru wamepungua sana.Kuna kiasi kikubwa cha uharibifu wa mazingira hapo, kuna RC mmoja simkumbuki, alisimamia sana zoezi la upandaji miti japo wenyeji wakawa wanalaani kazi hiyo kwa kisingizio kuwa miti inaleta kunguru
Nadhani Morogoro hali sio nzuri kabisa, impact yake ni kubwa sana na hasa ukizingatia kuwa iko karibu na jiji la Dar effect ya high population Dar inaonekana Morogoro.Wataalam wanasema Global Warming. Na huu ni mwanzo tu na watu wengi sana watakufa kwa hili joto hatarishi. Mvua pia zitakuwa ni kubwa sana kuliko ilivyo kawaida hivyo kuleta maafa makubwa sana sehemu mbali mbali
Duniani.
Sasa kunguru na mafuriko, ukosefu wa maji na joto kipi bora? Kunguru wanadhibitika mfano Dar es salaam kunguru wamepungua sana.
Hii nakubaliana nayo. Hivi ile kampeni ya kuzuia utengenezaji, uuzwaji na matumizi ya mkaa imefikia wapi? Au ndo imekufa kama zinavyokufa kampeni zingine zenye manufaa? Na uhamasishaji wa matumizi ya gesi umefikia wapi maana a gesi ndo zinazidi kupanda tuu.Nadhani ndio Mkoa unaoongoza kwa uuzaji wa mikaa! Wanakata sana miti kwa ajili ya kutengenezea mikaa.
Lushoto iliyokuwa inajulikama kama Geneva of Africa kuna mbu sasa hivi?? mi nimefika huko kabla ya 2000 kwa kweli kulikuwa kunapendeza sana.Nilikua Lushoto - Tanga last week, kuna joto na mbu balaaa. Sikuamini kabisa, eneo lililokua na Baridi Kali eti nimelala bila blanket?